Mkuu wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.
Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho, kukagua miundombinu yake. (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.
Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo
hicho, kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, injini ya
ndege inayotumika kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin
Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo
cha Usafirishaji (NIT).
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha Naibu Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, moja ya
kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya
chuo hicho.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya
kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
No comments:
Post a Comment