TANGAZO


Saturday, March 5, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA JIJINI MWANZA

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam juzi, wakati alipomtangaza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo , Mh. Nape Nnauye kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka mwaka huu, litakalofanyika  Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Machi 27, mwaka huu.

Waziri Nape Nnauye  amelipa heshima tamasha la Pasaka na amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo, la jijini Mwanza.

Mkurugenzi Msama amemshukuru Waziri Nape kwa kumtambua Mungu na kushiriki katika kazi hiyo ya Mungu siku hiyo, ya tarehe 27 Machi mwaka huu.
Akiongelea waimbaji ambao tayari wamethiitisha kushiriki katika tamasha hilo, amewataja baadhi yake kuwa ni pamoja na Upendo Nkone, Faustine Munishi, Ephraim Sekereti kutoka Zambia, Rose Muhando Jesca BM , Bony Mwaiteje na wengine wengi.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka juzi jijini Dar es Salaam.
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza  jambo mbele ya waandishi wa habari wakati alipozungumzia maandalizi ya Tamasha la Pasaka juzi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment