Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akipiga ngoma alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Golden
Jubelee Towers alipokuja kushiriki katika uzinduzi wa Video mpya ya Mshairi
Mrisho Mpoto inayoitwa Sizonje. Wengine Pichani ni Mrisho Mpoto, Dk. Mwaka na
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye akizindua rasmi video ya Sizonje. Kushoto kwake ni
Mrisho Mpoto.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akiinadi video ya Sizonje kwa wadau mbalimbali waliofika
kushuhudia uzinduzi huo. Nape aisema video hiyo inawakilisha serikali ya awamu
ya tano na utumbuaji wa majipu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Msichana Butogwa Charles
Shija aliyeongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Congcong Wang aliyeshika
nafasi ya pili kitaifa katika mtihani wakidato cha nne.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha ushujaa kwa kijana Salmin Selemani ambae
alifanya vibaya katika mtihani wa kidato
cha nne lakini hakukata tamaa na kujitokeza hadharani ili asaidiwe, Waziri Nape
amejitolea kumwendeleza kijana uyu. (Picha zote na Daudi Manongi)
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Nnauye amewataka watanzania kutumia utamaduni wetu kujenga nchi yetu.
Waziri nape ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa
video ya mshairi Mrisho Mpoto mbele ya wadau mbalimbali wa sanaa kutoka kila
kona ya jiji la Dar es Salaam waliofurika kuangalia uzinduzi huo ulioendana
sambamba na mada kubwa mbili za utamaduni na lugha na kauli mbiu ya Kufeli
elimu sio mwisho wa maisha.
“Serikali ya awamu ya Tano imejipanga vyema katika
kutumia utamaduni wa nchi yetu kushape vijana wetu wawe na morali,wajitambue
ili wafike mbali,tutatumia utamaduni huu kujenga nchi yetu kikamilifu kwani ni silaha
tosha kuvutia hata nchi nyingine.Maisha sio rahisi,ni kuvumilia,kutokata tamaa
na kuweka malengo.Safari tumeianza na tutafika mbali”Alisema Nape.
Pia Waziri uyo aliwataka watanzania kumuunga mkono
Mrisho mpoto na kutomkatisha tamaa kwani anamsaidia rais wa awamu ya Tano
Mhe.John Pombe Magufuli katika kutumbua majipu.Mbali na hilo alimshauri Mrisho
mpoto kwenda mikoani kwani hata uko kina Sizonje wapo wengi muwaonyeshe kwamba
iko njia kwa watu waliokata tamaa.
Kwa upande wake Mrisho mpoto aliwasii watanzania
kujenga taifa letu na pia tujenge Kiswahili na kukitumia kama ajira kwani ni lugha ya sita kwa sasa duniani.
“Lazima tujue kwamba Kiswahili ni lugha ya
kibiashara,tuangalie fursa zilizopo kupitia Kiswahili kujipatia ajira kwani
nchi kama Namibia, Zimbabwe wamepokea Kiswahili na wanaitaji kufundishwa zaidi
na kwa namna hii izi zote ni fursa kwani lugha imekuwa bidhaa sasa”Alisema
Mpoto.
Wakichangia katika mjadala uliopewa jina “kufeli
elimu sio kufeli maisha” Bw.Ruge Mutahaba alisema kufeli darasani kusikuzwe na
kuwataka vijana kutengeneza maono mapema kwani yatakuwa ndio mwongozo wa maisha
yao yote na yatawafanya vijana kutokata tama mapema.
“Vijana Mjifunze kuwasiliana,muwe
wabunifu,mjifunze kuwa na utaratibu wa kujifunza kitu kipya kila siku,pia
mtengeneze jamii ya watu ambao ni watatua matatizo na sio watumikaji tu kwani
kwenye matatizo ndo kwenye fursa zote,msiiachie serikali pekee kushughulikia
huduma za jamii bali tumieni mwanya huo kuanzisha za kwenu”Alisema Ruge.
Naye mwakilishi kutoka TBL Bw George Kavishe
aliwataka vijana kujua mihimili yao pamoja na uwezo wao na kwa kufanya ivyo
watakuwa wamejua wapi wanacho na nini kinafaa kufanya ili kuboresha maisha yao.
Mjadala huo pamoja na uzinduzi wa video ya sizonje
uliambatana na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe.Nape kuwapa
vyeti vya pongezi na ushujaa vilivyoandaliwa na Mrisho Mpoto wanafunzi
waliofanya vizuri na wale waliofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne.
No comments:
Post a Comment