Mfanyabiashara tajiri wa Iran, Babak Zanjani, amepatikana na hatia ya ufisadi, na kuhukumiwa kifo.
Bwana Zanjani alikamatwa mwaka wa 2013, baada ya kutuhumiwa kuwa alichukua dola bilioni moja nukta 9 za pato la taifa, kutokana na mafuta.
Alikanusha tuhuma hizo.
Bwana Zanjani alisusiwa na Marekani na Umoja wa Ulaya, kwa kuisaidia serikali ya Iran na makampuni kadha, kuhepa vikwazo vya kiuchumi vya wakati huo, dhidi ya mafuta kutoka Iran.
Alikiri kuwa alitumia makampuni kadha katika Umoja wa falme za Imarati, Uturuki na Malaysia, kuuza mamilioni ya mapipa ya mafuta ya Iran, kwa niaba ya serikali.
No comments:
Post a Comment