TANGAZO


Sunday, March 6, 2016

Watu 12 wauawa katika vita Afrika ya Kati

Image copyrightAFP
Image captionWatu 12 wauawa katika vita Afrika ya Kati
Takriban watu 12 wameuaua katikamapigano yaliyotokea katika vijiji ndani ya Jamhuri ya Afrika ya kati.
Huu ni uvamizi wa kwanza na mauaji tangu Faustin-Archchange Touadera kuchaguliwa kama rais mapema wiki jana.
Mashambulizi hayo yalifanyika karibu na mji wa Bambari ulioko maeneo ya kati ya Jamhuri ya Afrika ya kati.
Maafa hayo yalisababishwa na wizi wa mifugo au mapigano ya kikabila la fulani.
Maafisa wa serikali walisema hakuna dalili inayoonyesha kwamba mapigano hayo yalisababishwa moja kwa moja na uhasama wa wa kisiasa, kijamii na kidini.
Image copyright
Image captionMapigano yalizuka Jamhuri ya Afrika ya kati mwaka wa 2013.
Mapigano baina ya makundi yanayounga pande hasimu za kisiasa yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine wengi wakiwachwa bila makao tangu mapigano yazuke mwaka wa 2013.
Katika uvamizi huu wa hivi karibuni, maafisa wa serikali waliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu 6 waliuaua kwenye vijiji tofauti siku ya jumamosi.
Diwani wa sehemu hiyo na kiongozi mmoja wa kundi la vijana katika eneo hilo waliambia Reuters kwamba wanawake watatu kutoka jamii moja walichinjwa kutoka umbali wa kilomita sita karibu na mji wa Amassaka Topi.
Image copyrightAFP
Image captionMji wa Bambari umekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara mwaka jana licha ya kuwepo vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani.
Mahakama ya kikatiba iliidhinisha ushindi wa aliyekuwa profesa wa hesabu Faustin-Archange Touadera siku ya jumanne baada ya awamu ya pili ya uchaguzi mnamo Februari 14, na kupeana mwanga wa kuapishwa kwake tarehe 25 mwezi huu.
Touadera ameahidi kutoa kipao mbele kwa urejeshwaji wa amani na kuwanyang'anya silaha makundi ya wanamgambo.
Mji wa Bambari umekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara mwaka jana licha ya kuwepo vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani.

No comments:

Post a Comment