Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John
Pombe Magufuli akizungumza na viongozimbalimbali toka Tanzania na Vietnam
kwenye halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang
iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza
na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John
Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong
Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika
halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akigonga glass na Mke wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang (kulia)
akiwa amenyanyua glass juu pamoja na Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ikiwa ni ishara ya kutakia heri kati ya Tanzania
na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John
Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya
Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang wakitoa heshima kwa nyimbo za mataifa hayo
mawili.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Aldof
Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na
Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspecta Generali Ernest Mangu, wa pili
kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama
Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna
Simon Sirro.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati)
akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong
Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Generali Abdulrahman
Shimbo. (Picha zote na Raymond Mushumbusi Maelezo)

No comments:
Post a Comment