Masoko manne ya ng'ombe ambayo ngombe za wizi zilikuwa zikiuzwa ili kufadhili kundi la wapiganaji la Boko haram yamefungwa.
Wapiganaji hao wamekuwa wakitumia maajenti kuuza ng'ombe zilizoibwa kulingana na gavana wa jimbo la Borno.Biashara ilisitishwa kwa kipindi cha wiki mbili katika soko la ngombe la Gamboru,ambalo ni miongoni mwa masoko makubwa Afrika.
Boko Haram limeiba ng'ombe wengi nchini Nigeria na taifa jirani la Cameroon.
Mashambulio ya miaka sita ya kundi hilo yamesababisha vifo vya watu 17,000,kuharibu shule 1000 na kuwawacha zaidi ya watu milioni mbili bila makao.
No comments:
Post a Comment