Rais Barrack Obama wa Marekani ataondoka katika ikulu ya White House mwaka 2017,lakini hatahamia mbali.
Bwana Obama alisema siku ya Alhamisi kwamba familia yake itahamia mjini Washington,huku mwanawe wa kike Sasha akimaliza shule katika Elite Academy,Sidwel Friends.''Kumhamisha mtu katikati ya mafunzo ni ngumu'', alisema alipokuwa akijibu maswali huko Wisconsin.
Sijambo la kawaida kwa marais kuishi katika mji mkuu baada ya kuondoka madarakani.
Woodrow Wilson ambaye alihudumu kama raia mwaka 1913 hadi 1921 alikuwa wa mwisho kufanya hivyo.
Hatahivyo familia ya Obama pia inapanga kuishi kwa mda mjini Chicago,ambapo familia ina nyumba na bi Michelle Obama ana familia yake.
Obama pia anaimarisha maktaba yake mjini Chicago.
No comments:
Post a Comment