Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (katikati) akizungumza na wasanii pamoja na wadau wa filamu (hawapo pichani) wakati wa kufungua kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu juzi Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba.
Wasanii na wadau wa filamu wakisikiliza kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu juzi Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi
(katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wasanii na wadau wa filamu nchini
juzi jijini Dar es Salaam baada ya kufungua
kikao
cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu
katika tasnia ya filamu. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi.
Joyce Fisoo na wapili kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon
Mwakifwamba. (Picha zote na Genofeva Matemu - Maelezo)
Na Genofeva Matemu – Maelezo
06/12/2015
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi wakati
wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na
kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu juzi Jijini Dar es Salaam.
“Kama Ilani ya mwaka 2015 – 2020
ilivyodhihirisha serikali itaendelea kuimarisha uwezo wa Bodi ya Filamu nchini
ili isimamie kwa ukamilifu utekelezaji wa sheria zinazohusu shughuli za filamu
na ubunifu kwa lengo la kulinda haki na maslahi ya wanatasnia wa filamu”
alisema Bibi Malemi.
Aidha Bibi. Malemi amewakumbusha
wasanii kutekeleza sheria, kanuni na
taratibu kwani ni wajibu wa kila mtu kutii bila shuruti na kuwataka kutambua ya
kuwa utekelezaji wa sheria hauna mbadala na siyo wa hiari.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Bibi. Joyce Fisoo amesema kuwa
kikao kazi cha wadau filamu kinatoa fursa kwa wadau wote wa tasnia ya
filamu kujifunza kutoka kwa wataalamu
mbinu mbadala za kimaendeleo pamoja na kutoa fursa ya kujitathmini wao wenyewe
ili kuweza kufikia azma yao na azma ya kuinua tasnia ya filamu nchini.
Naye msanii wa filamu nchini Bibi. Coletha
Raymond amesema kuwa kikao cha wadau wa filamu kimefanyika wakati muafaka na
kuviombavyombo husika pamoja na wasanii kushirikiana kuunganisha nguvu
kutekeleza yale watakayoyaainisha katika kikao hicho kinacholenga kuboresha
tasnia ya filamu nchini.
Bibi Coletha amewataka wasanii wasiwe
wabishi na kung’ang’ania kufanya kitu cha aina moja bali wawe wabunifu kwani mchango
wa wasanii umekua ukionekana katika matukio mbalimbali yakitaifa na yasiyo
yakitaifa.
No comments:
Post a Comment