TANGAZO


Sunday, November 1, 2015

Waandamana kupinga mauaji Bangladesh

Image copyrightAP
Image captionWaandamana kupinga mauji Bangladesh
Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka, kupinga mashambulio yaliyofanywa jana dhidi ya wachapishaji na watovuti.
Waalimu, waandishi, na wanafunzi, walikusanyika katika chuo kikuu cha Dhaka, siku moja baada ya genge, linaloshukiwa la wapiganaji Waislamu, kumdunga visu hadi kufa mchapishaji wa vitabu, na kuwajeruhi watu wengine watatu, wasiokuwa na msimamo kama wao.
Image copyrightap
Image captionWaalimu, waandishi, na wanafunzi, walikusanyika katika chuo kikuu cha Dhaka
Polisi wanasema, kundi hilo la Waislamu wa siasa kali, Ansarullah Bangla Team, walihusika na mashambulio ya jana, pamoja na mengine yaliyotokea mwaka huu dhidi ya watovuti.
Hapo kesho, maduka ya vitabu yatafungwa kwa nusu siku nchi nzima, kulalamika juu ya mashambulio hayo.

No comments:

Post a Comment