Urusi imesitisha safari zake zote za ndege kuelekea Misri - huku Marekani ikiimarisha usalama wake katika ndege zote zinazoelekea Misri.
Hatua hii imechukuliwa wakati ushahidi unapozidi kuimarika kuwa bomu ndilo lililolipua ndege iliyodondoka kutoka angani katika Rai ya Sinai juma moja lililopita.
Habari kutoka vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa maafisa wa ujasusi nchini Marekani walisikiliza habari za siri miongoni mwa viongozi wa kundi la wapiganaji la Islamic State nchini Syria kabla na baada ya ndege hiyo kuanguka.
Maafisa wa shirika la habari la NBC liliwanukuu maafisa ambao halikutaka kuwataja majina wakisema waliwasikia viongozi hao wa Islamic State wakijigamba jinsi walivyoiangusha ndege hiyo.
Ripoti nyingine iliyotangazwa na kituo cha televisheni cha Ufaransa cha France Deix zinasema kuwa mlipuko unasikika katika chombo cha kurekodi yanayotokea kwenye ndege wakati wa kuanguka kwake.
Maafisa wa uchunguzi wa Ufaransa wamekataa kuthibitisha ripoti hizo.
No comments:
Post a Comment