Chama cha CCM kimenyakua idadi kubwa ya viti vya wabunge maalum miongoni mwa vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita.
CCM kimejipatia viti 64, huku CHADEMA kijipatia viti 36 kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha Upinzani CUF nacho kimejipatia viti 10.
Akizungumza na waandishi wa habari,jaji Damian Lubuva aidha amesema kuwa idadi ya viti maalum vya wabunge wanawake imepanda hadi kufikia 40.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ,idadi hiyo imetolewa kwa vyama hivyo baada ya kukidhi vigezo vya katiba na sheria ya kupata asilimia tano ya kura zote halali za ubunge.
Amesema kutokana na uchaguzi huo CCM ilipata kura za ubunge milioni 8,333,953, huku CHADEMA ikipata kura 4,627,923 nayo CUF ikipata kura 1,257,051.
Jaji lubuva amesema kuwa kutokana na majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi ,mgawanyo wa viti maalum sasa ni 110 ambapo viti vitatu vilivyosalia vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
No comments:
Post a Comment