Mke wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA nchini Tanzania Edward Lowassa amekataa ombi la kamati ya chama hicho kumpatia ubunge wa viti maalum.
Taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na msemaji wa Lowassa Abubakar Liongo imesema kuwa bi. Regina Lowassa aliikataa nafasi hiyo kwa nia njema.
Bwana Liongo amesisitiza kuwa bi. Regina ataendelea kuwahudumia raia hususan wanawake hata ijapokuwa ameikataa fursa hiyo ya kuwa mbunge.
''Naishukuru kamati ya chama changu kwa kunipatia heshima hiyo lakini sijaikubali.Nadhani itakuwa nyema kwangu mimi kuendelea na harakati zangu kuwapigania raia hususan wanawake nikiwa nje ya bunge''alisema.
Kamati kuu ya CHADEMA ilimpatia nafasi hiyo kutokana na mchango wake katika kampeni ambao ulisaidia kupatikana kwa majimbo.
No comments:
Post a Comment