Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amekubali kwa moyo mkunjufu na wa huruma mechi kati ya England na Ufaransa itakayochezwa juma lijalo katika uwanja wa Wembley.
Hogson amesema licha ya maafa yaliyosababishwa na ugaidi, tutajianda ipasavyo ndani na nje ya uwanja huo wa Wembley.
''Huu ni wakati wetu kuonesha dunia kuwa kandanda kwa hakika inaweza kuunganisha ulimwengu.'' alisema Hogson.
''Ninaamini kuwa wachezaji wetu watajiandaa ipasavyo kuwaonesha wageni wetu kuwa Uingereza inaungana na Wafaransa wakati huu wa majonzi.
Mechi hiyo ya kirafiki itaendelea kama ilivyopangwa siku ya jumanne jioni licha ya msururu wa mashambulio ambayo yamewaua takriban watu 129.
Washambuliaji 3 wa kujitolea muhanga walifariki katika milipuko nje ya uwanja wa Stade de France huku wachezaji wa Ufaransa wakicheza dhidi ya Ujerumani siku ya ijumaa.
Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ambayo rais wa Ufaransa alilazimika kutoroshwa baada ya mashambulizi ya kujitolea muhanga
Lakini rais wa shirikisho la soka la Ufaransa FFF Noel le Gaet amesema kuwa Les Blues itasafiri mjini London.
Shirikisho la soka nchini Ufaransa limesema kuwa :kwa pamoja na shirikisho la soka la Ufaransa FFF tunaunga mkono uamuzi huo.
FA pia imesema kuwa mechi ya Uingereza itakayowashirikisha vijana walio chini wa umri wa miaka 20 dhidi ya Ufaransa siku ya jumamosi imeahirishwa.
No comments:
Post a Comment