TANGAZO


Sunday, November 15, 2015

Gari la pili la wavamizi lapatikana Paris


Image copyrightBFMTV
Image captionGari la pili lililotumika na wavamizi lapatikana Paris

Polisi wa Ufaransa wamelipata gari la pili linalofikiriwa lilitumika katika mashambulio ya Ijumaa usiku mjini Paris.
Gari hilo la aina ya Seat, lilipatikana limeachwa mashariki mwa jiji.
Aidha gari hilo liinavoripoitiwa lilikuwa na silaha.
Awali gari lilokodiwa Ubelgiji, lilipatikana hapo jana, karibu na ukumbi wa tamasha, ambamo waliuwawa wengi kati ya watu 129 waliokufa.
Watu watatu wamekamatwa mjini Brussels kwa kushukiwa kuhusika na mashambulio hayo.
Mmoja wa washambulizi waliotekeleza mauaji hayo ametajwa kuwa ni Omar Ismail Mostefai.

Image copyrightAFP
Image captionUlinzi bado ni mkali nchini Ufaransa, na wanajeshi 3,000 wanapiga doria mjini Paris

Raia huyo wa Ufaransa, alijulikana kwa wakuu wa kupambana na ugaidi , kwamba alikuwa Muislamu mwenye msimamo mkali.
Polisi wamewakamata jamaa na marafiki wake na wahoji .
Ulinzi bado ni mkali nchini Ufaransa, na wanajeshi 3,000 wanapiga doria mjini Paris, ambako makumbusho, majumba ya sanaa na maeneo yanayovutia watalii bado yamefungwa.
Nchi hiyo iko katika siku ya pili kati ya tatu za maombolezo, na sala ya wafu itafanywa leo.
Watu zaidi ya 300 walijeruhiwa katika mashambulio - na wengi bado ni mahatuti.
Hapo jana watu wa Paris walipanga foleni kwa saa kadha, wakisubiri kutoa damu bada ya ripoti kuibuka za upungufu wa damu kufuatia idadi kubwa zaidi ya majeruhi nchii humo kwa zaidi ya miaka 50.

Image copyrightReuters
Image captionWafaransa wanashauriwa wasiondoke makwao

Shahidi mmoja Michael O'Connor -- alikuwa katika mojawapo ya maeneo yaliyoshambuliwa katika tamasha la Bataclan
Ameelezea vipi yeye na mpenziwe walivyo lala kifudifudi kama vile wamefariki ndio wakasalimika .
Wakati huohuo,Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, anasema kuwa kati ya 20-30 ya wahanga wa mashambulizi hayo hawajatambuliwa.

No comments:

Post a Comment