Mjadala wa wagombea wa urais wa Marekani katika chama cha Democratic umekamilia katika jimbo la Iowa nchini humo huku Kinara wa chama hicho na waziri wa zamani mambo ya nje wa Marekani bi , Hilary Clinton,akisema ni sharti dunia ipambane na itikadi za kigaidi.
Hata hivyo mmoja wa wapinzani wake, Seneta Bernie Sanders, amemkosoa akisema sera ya Bi Clinton huko Iraq ndizo ziliyoijengea dunia mazingira ya kushamiri kwa makundi ya wapiganaji kama vile Al Qaeda na IS.
Bi Clinton akizungumza huko Iowa alisema swala la ugaidi sio vita vya wamarekani pekee.
Aliwataka viongozi wa mataifa ya kiarabu kufanya kazi ya ziada kupunguza mfumo unaozalisha ugaidi zaidi.
Clinton alizitaka Uturuki na mataifa ya Ghuba kusaidia kutatua tatizo la ugaidi.
Mpinzani mwengine Martin O'Malley alipinga ushauri wa bi Clinton akidai sharti Marekani ijitwige jukumu la kupambana na ugaidi wala sio kufwata ushauri wa Bi Clinton.
Siku ya Ijumaa magaidi walivamia maeneo sita mjini Paris na kuwaua takriban watu 129 watu zaidi ya mia tatu wanauguza majeraha mabaya ya risasi.
Wadadisi wa kisiasa wanasema mashambulizi hayo ya Ufaransa bila shaka yatabadili mwelekeo wa mjadala huo huku maswala ya usalama wa ndani ya nchi yakipewa kipao umbele.
Mjadala huo ulianza kwa watu kukaa kimya kwa mda kuwakumbuka wahanga wa mashambulio ya huko Paris.
No comments:
Post a Comment