Sony Masamba akichana mistari na mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuzirudi huku Joniko Flower, Sam Mapenzi na Kasongo Junior wakimsikindiza kwa miondoko ya aina yake. Hakika hii sio ya kukosa leo Jumapili.
Kasongo Junior na Suzy wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita, bila kukosa ya leo itakuwa pale pale.
Kasongo Junior na Suzy wakiendelea wakizirudi kwenye kiota cha Escape One.
Sam Mapenzi akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Jumapili iliyopita ndani ya kioa cha Escape One Mikocheni ambapo leo pia burudani iko pale pale na ndio kwanza week end imeanza kwa fans wa Skylight Band.
Waimbaji wa bendi ya Skylight, Joniko Flower na Sony Masamba wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao ndani ya kioata cha Escape One Mikocheni jijini Dar.
Sam Mapenzi na Sony Masamba wakiendelea kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band.
Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower akiwasebenesha sehemu ya mashabiki wao Jumapili iliyopita kwenye Skylight Sunday Bonanza kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Joniko Flower akizirudi pamoja na Mashabiki wa Bandi ya Skylight pamoja na waimbaji wa bendi hiyo.
Suzy akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Escape One jumapili iliyopita.
Waimbaji wa Bendi ya Skylight wakiendelea kutoa burudani huku wakiongozwa na Rapa Mkongwe wa muziki wa dansi wa Skylight Band, Joniko Flower.
Kifaa kipya cha Bandi ya Skylight, Leah akitoa burudani ya nguvu mbele ya mashabiki wao huku akisindikizwa na Kasongo Junior.
Waimbaji wa Bendi ya Skylight pamoja na mashabiki wa bendi hiyo wakiendelea kuzirudi katika kiota cha Escape One Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment