TANGAZO


Sunday, November 15, 2015

Wanafunzi Kisarawe wapigwa msasa wa elimu ya Usalama barabarani

 *Ni katika kuadhimisha siku ya wahanga wa ajali za barabarani duniani
Askari wa Jeshi la Usalama barabarani  Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Koplo Alphonce Mnibi (kushoto)  akimuelekeza mwanafunzi wa darasa la tano  wa  shule ye msingi  Chanzige A,  John Khamsini jinsi ya kuwavusha  wanafunzi wenzake  pindi  wanapovuka  barabara , mafunzo hayo yalifanyika  shuleni hapo kwa udhamini wa vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha  siku ya wahanga wa ajali barabarani  duniani iliyofanyika jana. 
Mwanafunzi wa shule ya msingi Chanzige A, John Khamsini (kulia) akionyesha kibao cha kuvushia wanafunzi wenzake huku askari wa Usalama barabarani Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Koplo Alphonce Mnibi   akiwaelekeza jinsi ya kuvuka na mwanafunzi wa shule hiyo Azizia Mzige.Mafunzo hayo  maalum kwa wanafuzi hao yaliendeshwa na Jeshi hilo kwa kushirikiana na  Vodacom Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wahanga wa ajali za barabarani duniani iliyofanyika  jana. Katikati ni Mrakibu msaidizi wa polisi wa Wilaya hiyo, Saumu Mgagi na Koplo Bonda Semule. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Chanzige A, Wilaya ya  Kisarawe mkoa wa Pwani, wakimsikiliza kwa makini askari wa Jeshi la Usalama barabarani, Koplo  Alphonce  Mnibi , wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya njinsi ya kuvuka barabara kwa wanafunzi hao , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wahanga wa ajali za barabarani  duniani iliyofanyika jana.Mafunzo hayo yaliendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania. 
Askari wa Jeshi la Usalama barabarani  Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Koplo Alphonce Mnibi  akiwaonyesha alama za barabarani baadhi ya  wanafunzi wa  shule ya msingi  Chanzige A,  Kisarawe, Wakati wa mafunzo maalum ya kuvuka barabara   kwa wanafunzi  yaliyoendejeshi hilo kwa kushirikiana Vodacom Tanzania katika kuadhimisha siku ya wahanga wa ajali za barabarani duninani yaliyofanyika hapo jana.  

Askari wa Jeshi la Usalama barabarani  Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Koplo Alphonce Mnibi akiwashuhudia baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Chanzige A, iliyopo wilaya ya Kisarawe  mkoa wa Pwani ,wakiongozwa na  mwanafunzi mwenzao, John Khamsini jinsi ya kuvuka barabara,baada ya kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wahanga wa ajali za barabarani duninani yaliyofanyika hapo jana. Mafunzo hayo yaliendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na  Vodacom Tanzania.

Na Mwandishi wetu
KATIKA kuazimisha siku ya wahanga barabarani duniani jana wanafunzi wa shule ya Msingi Chazinge A iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani wamenufaika kwa kupatiwa elimu ya usalama barabarani kutoka Jeshi polisi la Usalama barabarani kwakushirikiana na Vodacom Tanzania.

Elimu hiyo imetolewa jana katika kuadhimisha siku ya wahanga wa ajali za barabarani ambayo huadhimishwa Novemba 15 kila mwaka na wanafunzi walipata fursa ya kujifunza alama muhimu za barabarani na matumizi ya barabara na mambo muhimu ya kuzingatia kuwaepushia ajali wanapokuwa wanatumia barabara wakati wa kwenda na kutoka shuleni na matembezi mengineyo.

Akiongea kuhusiana na siku ya wahanga wa ajali za barabarani Mrakibu Msaidizi wa Kituo cha Polisi cha Kisarawe Saumu Mgagi ameipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada  za serikali katika kutokomeza ajali  za barabarani “Kwa kutoa elimu hii kwa watoto wadogo  waliopo mashuleni kwa kiasi kikubwa tutaweza kupunguza tatizo hili kwa kuwa wataendelea kukua wakijua matumizi sahihi ya barabarani na kwa upande wao ni rahisi kuelewa kuliko watu wazima.

Siku ya wahanga wa ajili za barabarani huadhimishwa duniani kote ambapo taasisi mbalimbali zinazohusika na kupambana na ajali huitumia kutoa elimu kwa jamii kama ambavyo imefanya Vodacom.Kauli mbiu ya siku hii kwa mwaka huu ni “Ni wakati wa kukumbuka sasa –Sema  Hapana kufanya uhalifu wa barabarani”.

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania  Rosalynn Mworia amesema kuwa suala la kuelimisha jamii kuhusiana na usalama barabarani ni  jambo ambalo kampuni ya Vodacom itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiaa na Jeshi la Polisi na wadau wengine.

“Tatizo la ajali nchini ni kubwa na kila mwaka wananchi wengi hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ikiwemo idadi kubwa ya watu kubaki wakiwa na ulemavu wa aina mbalimbali pia ajali zinaathiri familia nyingi kutokana na wategemezi katika familia kupoteza maisha ama kupata ulemavu kutokana na ajali hususani za barabarani”.

Alisema tatizo hili ili kulitokomeza linahitaji ushirikiano wa watu wote “Vodacom tumekuja na mikakati mbalimbali ya kufanya kampeni hizi mojawapo ikiwa kupeleka elimu ya usalama barabarani kwa watoto wadogo waliopo mashuleni kama tulivyofanya leo na mkakati huu unaendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali”.Alisema.

Mworia alisema mbali na elimu mashuleni Vodacom kwa kushirikiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani imekuwa ikiendesha kampeni ya “Wait to Send” ambayo inahamasisha  madereva wanaoendesha vyombo vya moto kutotumia simu za mkononi wanapokuwa barabarani na kutotumia vinywaji vyenye kilevi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto kwa ajili ya kulinda usalama wao,abiria wanaowabeba na watumiaji wengine wa barabara.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Chazinge,Bw.Chande Chande alishukuru jeshi la polisi na Vodacom Tanzania kwa kupeleka elimu ya usalama barabarani shuleni hapo kwa kuwa imewawezesha wanafunzi na walimu kujifunza mambo mengi kuhusiaana na matumizi sahihi ya barabara kwa usalama wao “Tunashukuru kwa kutukumbuka na kutuletea elimu hii muhimu ya usalama barabarani na wanafunzi wameipokea vizuri na kwa kiasi kikubwa itawasaidia  kuepuka ajali  wanapokuwa wanatumia barabara”.Alisema.

No comments:

Post a Comment