Pages

Saturday, September 26, 2015

Simba yakubali kwa Yanga, yapigwa bao 2-0 Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo

Mashabiki wa Yanga wakicheza ngoma wakati wa mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba Uwanjwa wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 2-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mshabiki wa Simba wakionesha bango lililokuwa likionesha timu yao kuendelea kuichapa Yanga mabao 3-0, kabla ya mchezo huo leo. 
Mashabiki wa Yanga wakiwa wameduwaa mara baada ya kuanza kwa mchezo kati ya Yanga na Simba ambapo mashabulizi ya mara kwa mara yalikuwa yakielekea golini kwao.
Mussa Hassan 'Mgosi' wa Simba, akijaribu kutaka kumpiga chenga Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga katika mchezo huo. 
 Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Yanga.
Golikipa Ally Mustafa 'Bathez' akidaka mpira uliokuwa ukifuatwa na Hamis Kiiza wa Simba (mbele yake), wakati wa mchezo huo. 
Mashabiki wa Simba wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya timu yao kuelemewa mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kipindi cha pili kwa jumla. 
Mbuyu Twite (kulia) na Haruna Niyonzima wote wa Yanga wakipongezana baada ya Malimi Busungu kuifungia timu yao bao la pili katika mchezo huo. 
Ally Mustafa 'Berthez', wa Yanga, akidaka kiatu cha Hamis Kiiza wa Simba, wakati wa purukushani kwenye lango la timu hiyo.
Malimi Busungu wa Yanga wakipambana na Simon Sserunkuma wa Simba. 
Mashabiki wa Yanga wakionesha vidole viwili na wengine vitatu kuashiria ushindi wa timu yao dhidi ya Simba, kabla ya kupigwa mchezo huo, wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 2-0. 
Mashabiki wa Yanga wakimuangalia mwenzao, aliyejiandika mgongoni jina la mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.  
Kijana shabiki wa Yanga, akionesha alama ya kuchinja na vidole vitatu, akimaanisha timu yao kuichapa Simba katika mchezo huo. 
Kijana shabiki wa Yanga, akionesha alama ya kuchinja na vidole viwili, akimaanisha timu yao kuichapa Simba katika mchezo huo. 
Mwinyi Kazimoto wa Simba akiudhibiti mpira huku akiangaliwa na Nadir Haroub 'Canavaro' (kulia), wakati wa mchezo huo. 
Mashabiki wa Yanga wakifurahia bao la kwanza la timu hiyo. 

Kikosi cha timu ya Yanga kilichoshuka dimbani kupambana na Simba leo. 
Kikosi cha timu ya Simba kilichoshuka dimbani kupambana na Yanga leo.  
Ubao wa matokeo ulivyokuwa mara baada ya kuanza mchezo huo. 
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga bao 1 lililopatikana katika dakika ya 43 ya kipindi cha kwanza. 
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga mabao 2 mpaka dakika ya 48 ya kipindi cha pili (dakika ya 93) ya mchezo huo. 

No comments:

Post a Comment