TANGAZO


Saturday, August 8, 2015

Mamia wamzika babake mtoto aliyetekezwa

Mamia wajitokeza kumzika Saad Dawabsha katika ukingo wa Magharibi Palsetina

Mamia ya wakazi wa ukingo wa Magharibi (West Bank) unaokaliwa na Israeli wamejitokeza kwa mazishi ya babake mtoto wa kipalestina aliyeteketezwa hadi akafa na walowezi wa kiyahudi.
Sa'ad Dawabsheh aliaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli alikokuwa akipokea matibabu baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili wake.
Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.

Dawabsheh alimpoteza mwanawe juma lililopita alipoteketea ndani ya nyumba yao

Mke wake bi Riham na mwana wao wa kiume Ahmad bado wako katika hali mahututi hospitalini.
Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikia
usalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin aliahidi kuwa wale waliotekeleza kitendo hicho alichokitaja kuwa cha kigaidi wangechukuliwa hatua za kisheria.
Netanyahu alielezea mshangao wake kutokana ni kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili alipowatembelea wazazi wa mtoto huyo na nduguye hospitalini.

Mke wake bi Riham na mwana wao wa kiume Ahmad bado wako katika hali mahututi hospitalini.

Hakuna mtu aliyekamatwa kufikia sasa kufuatia shambulizi hilo.
Afisa wa Palestina, Ghassan Daghlas, alisema walowezi wa Israil, walichoma moto nyumba nyengine katika kijiji cha Duma hii leo, lakini hakuna mtu aliyeumia vibaya.
Umoja wa Mataifa unasema walowezi wa Israil wamefanya mashambulio kama 120 mwaka huu, katika Ufukwe wa Magharibi uliokaliwa.
Msemaji mmoja wa kundi la Hamas amewataka wapalestina walipize kisasi kufuatia shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment