TANGAZO


Saturday, August 8, 2015

China yawahamisha Maelfu ikihofia kimbunga



Soudelor ilisababisha hasara kubwa kutokana na kasi ya upepo

Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka kusini-mashariki mwa China wakati taifa hilo linajiandaa kwa kuwasili kwa kimbunga kinachokaribia.
Mji wa Fujian, ulioko katika pwani ya nchi hiyo, limetoa tahadhari kubwa kabisa ya kimbunga na kuonya kuwa ni tishio kubwa sana.
Kimbunga cha Soudelor kilisababisha matafaruku nchi jirani ya Taiwan.

Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka Musini-Mashariki mwa China

Soudelor ilisababisha hasara kubwa kutokana na kasi ya upepo kuwa zaidi ya kilomita 230 kwa saa.
Kiliangusha miti na kuporomosha mapaa na mabango makubwa.
Mabarabra mengi tayari yamefungwa kwa miti iliyong'olewa na kuachwa barabarani.

Mabarabra mengi tayari yamefungwa kwa miti iliyongolewa na upepo

Safari za treni na ndege zilivunjwa na shule na maofisi yalifungwa.
Mamilioni ya nyumba zinakosa umeme.

No comments:

Post a Comment