TANGAZO


Monday, August 10, 2015

Mafunzo kwa wachimbaji wa madini kuhusu matumizi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao-Kanda ya Ziwa Nyasa-Songea tarehe 7/8/2015 na Tunduru 9/8/2015

Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini-Kitengo cha Leseni, Idd Mganga (kushoto aliyesimama) akielezea Historia ya utoaji Leseni za Madini nchini  wakati wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Songea. Wa kwanza kulia ni Mtaalamu kutoka Kitengo hicho, Mhandisi Edward Mumba na anayemfuatia ni Mhandisi George Wandibha wa Ofisi ya Kanda ya Madini Songea. 
Baadhi ya wachimbaji Madini wa Songea wakimsikiliza Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa mafunzo hayo ya Mjini Songea.  
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idd Mganga akiendelea na mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ufundi (VETA), mjini Songea.  
Ofisa Madini Mkazi Tunduru, Mhandisi Frederick Mwanjisi akifungua mafunzo hayo kwa wachimbaji madini yaliyofanyikia katika ukumbi wa Clasta wilayani Tunduru. 
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiwaelekeza wachimbaji wadogo wa wilayani Tunduru namna Mfumo wa Huduma ya Leseni kwa njia ya Mtandao unavyofanya kazi. Wa Kwanza kushoto ni Idd Mganga na anayemfuatia ni Mhandisi Edward Mumba. 
Mchimbaji mdogo wa Wilayani Tunduru, Mwajuma Omari akitoa shukrani kwa niaba ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo hayo kwa Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini hawapo pichani.

Na Mwandishi wetu
WIZARA ya Nishati na Madini inaendelea na mpango wake wa Mafunzo kwa Wachimbaji Madini Nchini kuhusu matumizi ya Mfumo wa Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao yaani Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).

Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokea malipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa wachimbaji wadogo nchi nzima ili kuwajengea uwezo.

No comments:

Post a Comment