Ofisa wa Polisi akiwasili Ofisi Kuu za CUF, kuonana na viongozi wa umoja huo kwa ajili ya kupanga msafara wa mgombea huyo, viongozi wa ukawa, wanachama, wananchi pamoja na mashabiki wa mgombea huyo, kuelekea ofisi za NEC, Posta Mpya, jijini leo.
Baadhi ya Askari Polisi wa Kikosi maalum cha kutuliza ghasia wakiwa ofisini hapo leo kwa ajili ya kufuatilia msafara huo.
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Ukawa, kupitia Chama cha Chadema, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, akiwasili Ofisi za CUF, Buguruni tayari kuanza msafara wa kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo.
Msafara wa kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo ya mgombea wa Ukawa, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ukianza leo asubuhi.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa katika msafara huo.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akiwa katika msafara huo.
Wananchi, wanachama Vyama vya umoja wa Ukawa na mashabiki wa mgombea huyo, wakielekea ofisi za NEC, Posta Mpya, jijini leo kumsindikiza mgombea huyo.
Wananchi, wanachama Vyama vya umoja wa Ukawa na mashabiki wa mgombea huyo, wakielekea Ofisi za NEC, Posta Mpya, jijini leo kumsindikiza mgombea huyo. Mbele katikati ni wanandugu, Suleiman Khamis Ally (katikati) na mdogo wake, Masoud Said Ally (kushoto), kutoka Pemba, wakiwa katika msafara huo.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye moja ya jengo linaloendelea kujengwa Barabara ya Uhuru karibu na Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, wakiangalia msafara huo.
Umati wa wananchi, wanachama Vyama vya umoja wa Ukawa na mashabiki wa mgombea huyo, wakielekea Ofisi za NEC, Posta Mpya, jijini leo kumsindikiza mgombea huyo.
Baadhi ya mashabiki wa mgombea huyo, wakipozi kwa picha wakati wa msafara huo.
Baadhi ya mashabiki wa mgombea huyo, wakipozi kwa picha wakati wa msafara huo.
Baadhi ya wananchi, wanachama Vyama vya Umoja wa Ukawa na mashabiki wa mgombea huyo, wakiwa kwenye gari la wazi, wakielekea Ofisi za NEC, Posta Mpya, jijini leo kumsindikiza mgombea huyo.
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Ukawa, kupitia Chama cha Chadema, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, akiwasili Ofisi za NEC, maeneo ya Posta Mpya, tayari, kwenda kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo.
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Ukawa, kupitia Chama cha Chadema, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (katikati nyuma), akipanda ngazi kuelekea Ofisi za NEC, maeneo ya Posta Mpya, tayari, kwenda kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi hiyo.
Ofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Deogratius Nsanzugwako, akimkabidhi mgombea wa nafasi ya Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, fomu za uteuzi kwa nafasi hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wa mgombea huyo, Regina Lowassa na kulia kwake ni mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji.Umati wa wananchi na wanachama Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakimsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais wa umoja huo, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, alipowasalimia wakati akitoka Ofisi za Tume ya Tafa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu za uteuzi, Dar es Salaam leo.
Umati wa wananchi na wanachama wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakifurahia wakati mgombea wa nafasi ya Urais wa umoja huo, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, alipokuwa akiwahutubia, Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo, alipokuwa akitoka Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu za uteuzi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, Onesmo ole Nangole, aliyejiengua na kujiunga na Chadema, akinyanyuliwa mkono na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Zanzibar, Kinondoni leo.
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Umoja huo, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, alipokuwa akiwahutubia, wananchi na wanachama wa Vyama vya umoja huo, Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo, alipokuwa akitoka Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuchukua fomu za uteuzi.
No comments:
Post a Comment