Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe akielezea mikakati ya Wizara katika uboreshaji wa huduma za leseni kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) katika mafunzo yaliyofanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.
Baadhi ya wachimbaji wa madini kutoka wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani).
Mmoja wa wachimbaji wa madini kutoka wilayani Same, mkoani Kilimanjaro Richard Mbwambo akiuliza swali katika mafunzo hayo.
Ofisa Madini Mkazi, Mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando akielezea sheria na kanuni za uchimbaji wa madini nchini katika mafunzo hayo.
Mmoja wa wachimbaji wadogo, Naamin Samuel kutoka kampuni ya Kivoroi na Ndarauoi akiuliza swali katika mafunzo hayo.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Uhasibu Erick Mkumbo akifafanua jinsi ulipaji wa leseni za madini unavyofanyika.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo waliosimama nyuma.
Baadhi ya watoto kutoka wilayani Same mkoani
Kilimanjaro wakipozi katika picha ya pamoja mbele ya gari la matangazo la Wizara ya Nishati na
Madini lililokuwa linatumika wakati wa zoezi la uhamasishaji wa matumizi
ya huduma za leseni za madini kwa
njia ya mtandao.
No comments:
Post a Comment