TANGAZO


Saturday, July 25, 2015

Rais Jakaya Kikwete awa mgeni rasmi Siku ya Mashujaa, Makamu wake, Dk. Bilal ashiriki maadhimisho hayo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal kulia, akiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kwenye maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyoadhimishwa leo Julai 25, 2015 katika viwanja vya Mmazi Mmoja Dar es Salaam. 
(Picha zote na OMR)

Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikiwa katika ukakamavu wakati wa kuweka silaha mbalimbali kwenye Mnara wa Mashujaa, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wastaafu wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa viwanjani hapo leo.
Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipuliza tarumbeta katika hayo, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka ngao katika Mnara wa kumbukumbu kwenye maadhimisho ya siku ya ya Mashujaa iliyoadhimishwa leo Julai 25, 2015 viwanja vya Mmazi Mmoja Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam baada ya kukamilika kwa maadhimisho ya siku ya Mashujaa leo Julai 25,2015. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama alipowasili viwanja vya Mmazi Mmoja, Dar es Salaam leo Julai 25,2015 kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha siku ya Mashujaa.

No comments:

Post a Comment