Na Mwandishi
Wetu
MTOTO mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa
ushauri wa kujijengea uwezo wa
kujiamini anayezidi kujipatia umaarufu
mkubwa duniani, Lonnie Hudson maarufu kama ‘King Nahh’(pichani), ametua jijini Dar es Salaam leo.
King Nahh
aliambatana na baba yake mzazi Nyeeam Hudson
ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa
taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
Kesho mtoto huyo, atafanya kongamano kubwa la watoto na wazazi katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za watu ambao wamekata tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.
“Najisikia
furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza
kubadili hisia zao, kujiamini na
kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.
King Nahh
aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia
kulaumu matatizo na vikwazo bila
kutafuta suluhu ya matatizo yao.
“Kila mtu
analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita.
Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila
ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii
ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda
kumlaki.
Mkurugenzi
wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa
ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili
waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.
“King Nahh
ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na kipawa
alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho Urafiki,
ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza
mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,” alieleza Henjewele.
HABARI KATIKA PICHA
King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Akikabidhiwa shada la mauwa uwanjani hapo.
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari.
King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni.
King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege.
Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.
Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi.
Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket.
Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce 'Dotnata'.
Akikabidhiwa 'token' na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa katika kipindi atakachokuwa nchini. Pembeni yake ni mratibu wa kongamano, Cynthia Henjewelle.
Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket.
Akijichagulia bidhaa.
No comments:
Post a Comment