TANGAZO


Saturday, July 25, 2015

Aysharose, Mlata waibuka kidedea

*Wema ashukuru wajumbe, asema ndio kwanza safari ya siasa imeanza
Aysharose Mattembe akishukuru wapiga kura wake mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida kupitia CCM.
Wagombea Ubunge wa Viti maalum Mkoa wa Singida Matha Mlata (kushoto) na Aysharose Mattembe mara baada ya kutangazwa kuwa kuwa washindi katika uchaguzi mkuu wa UWT jana. 
Msanii wa filamu, Wema Sepetu akiwapungia mkono wa shukrani wajumbe wa mkutano Mkuu wa UWT Mkoa wa Singida, mara baada ya mchakato huo wa uchaguzi wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum jana. (Picha zote na Hillary Shoo)

Na Hillary Shoo,
SINGIDA.
MKUTANO Mkuu wa uchaguzi wa Jumiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Singida umemchagua kwa kishindo Aysharose Matembe (311)na Martha Mlata (253) kuwa wagombea nafasi ya Ubunge wa Viti maalumu Mkoa wa Singida.

Katika uchaguzi uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Mjini hapa msimamizi mkuu wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone, mara baada ya kumtangaza Aysharose Ukumbi mzima ulilipuka kwa nderemo na vifijo.

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kipindi kilichopita Diana Chilolo alipata kura 182, akifuatiwa na msanii Wema Sepetu kura 90, na Sara Mwambu (74).

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Martha Gwao (44), Rehema Madusa( 24), Aziza Ntandu (5), Mary Marco (3), Sefa Josephine( 2). Salome Mpondo (1),Leah Samike(1) na Elizabeth Lucas (0).

Wakizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ,Wema Sepetu ambaye alikuwa kivutio kikubwa katika uchaguzi huo huku wajumbe wakiomba kupiga picha na msanii huyo ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006, alisema anashukuru kwa kupata kura 90 kwa kuwa ndio anaanza safari yake ya siasa.

Kwa upande wake Chilolo alisema anashukuru wapiga kura wake kwa kura alizopata kwani hiyo ni sehemu ya changamoto za uchaguzi na amekubali matokeo.

No comments:

Post a Comment