Timu za Azam FC ya Tanzania na Adama City ya Ethiopia zikiingia uwanjani tayari kwa mpambano wao, katika mchezo wa Kombe la Kagame, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wachezaji wa timu za Azam FC ya Tanzania na Adama City ya Ethiopia wakisalimiana kabla ya mpambano wao, huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa timu za Azam FC ya Tanzania na Adama City ya Ethiopia wakisalimiana kabla ya mpambano wao, huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Kikosi cha Adama City.
Kikosi cha Azam FC.
Makocha wa timu ya Azam, Stewart Hall (kulia) na akiwa na msaidizi wake.
Kipre Tchetche akipiga krosi kuelekea langoni mwa Adama City huku akizuiwa na Eshetu Menna wa timu hiyo.
Kipre Tchetche wa Azam FC, akijaribu kumpita na mpira Moges Tadese wa Adama City.
Moges Tadese wa Adama City, akiuzuia mpira, uliokuwa ukimilikiwa na Kipre Tchetche wa Azam FC.
Wachezaji wa Azam wakishangilia kwa kupongezana baada ya kupata bao la kwanza kwa timu yao hiyo dhidi ya Adama City ya Ethiopia, wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia kwa kucheza ndombolo baada ya kupata bao la kwanza kwa timu yao hiyo dhidi ya Adama City ya Ethiopia, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Kipre Tchetche wa Azam FC, akimruka Moges Tadese wa Adama City.
Wachezaji wa Azam wakishangilia kwa kupongezana baada ya kupata bao la pili kwa timu yao hiyo dhidi ya Adama City ya Ethiopia. Azam ilishinda mabao 5-0 katika mchezo huo.
Suleiman Mohamed wa Adama City, akiudhibiti mpira huku akizongwa na Ammy Ally wa Azam.
Erasto Nyoni wa Azam FC, akijaribu kumpita na mpira Moges Tadese wa Adama City.
Mashabiki wa Azam wakishangilia timu yao hiyo, wakati wa mchezo huo.
Ubao wa matangazo ukionesha matokeo ya mchezo huo baada ya kumalizika kipindi cha kwanza. Hadi mwisho wa mchezo Azam FC iliibuka kidedea kwa kuchapa Adama City kwa mabao 5-0.
No comments:
Post a Comment