TANGAZO


Tuesday, July 21, 2015

Marekani yazungumzia uchaguzi Burundi

Zoezi la upigaji kura laendelea Burundi
Marekani imesema uchaguzi wa Rais unaofanyika nchini Burundi umekosa uaminifu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za nje wa Marekani John Kirby amesema zoezi hilo la uchaguzi lililogubikwa na utata ambao utaendelea kuipunguzia sifa serikali.
Pierre Nkurunzinza anawania awamu ya tatu madarakani, licha ya awamu mbili za kukaa madarakani zilizowekwa kwa mujibu wa katiba.
Wagombea wengi kupitia vyama vya upinzani wamesusia uchaguzi huo. Wakati huohuo katika kijiji cha Buye kaskazini mwa nchi, alikozaliwa Rais Nkurunziza mlolongo wa watu wamejitokeza kupiga kura.

No comments:

Post a Comment