TANGAZO


Tuesday, July 21, 2015

Kenyatta: Hatutajadili jinsia moja

Maswala la mapenzi ya jinsia moja hayajaratibiwa katika mazungumzo baina yake na mgeni wake mashuhuri rais wa Marekani Barack Obama.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa maswala la mapenzi ya jinsia moja hayajaratibiwa katika mazungumzo baina yake na mgeni wake mashuhuri rais wa Marekani Barack Obama.
Rais Kenyatta aliyasema hayo katika hotuba kwa waandishi wa habari kuhusu ratiba ya rais Obama nchini humo.
Kenyatta alisema kuwa yeye anatarajia kumpokea rais Obama siku ya ijumaa na kuwa
Kenyatta akariri kuwa hatambagua naibu wake William Ruto
''hilo sio moja kati ya maswala yaliyopangiwa kuzungumziwa''
''Kama wakenya tiaf letu linakabiliwa na changamoto nyingi tu nafikiri tunamaswala ya muhumi zaidi ya kujadiliwa mbali na hilo la mapenzi ya jinsia moja'' alisema rais Kenyatta akijibu swali alilorushiwa na mwanahabari.
Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Kenya.
Rais Obama anatarajiwa kuzuru Kenya baadaye wiki hii
Kabla ya kujibu maswali ya waandishi wa Habari rais Kenyatta alikuwa ameisifu taifa lake kwa kuwa mwenyeji wa kongamano la wajarsiria mali ''Global Entrepreneurship Summit'' (GES) akisema hii ni mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa kusini mwa jangwa la sahara.
''Hii ni fursa nzuri na kubwa kwa wajasiria mali wakenya kukutana na kubadilishana mawazo na wenzao wa kimataifa'' alisema Kenyatta.
Vijana wetu bila shaka wameweka kigezo cha ubora katika ujasiria mali na ubunifu hata kuvutia mabwenyenye wa kimataifa wanaotafuta sekta za kuwekeza''aliongezea bwana Uhuru.
Ndege ya rais Obama imetua katika chuo kikuu cha Kenyatta
Mbali na hayo bwana Kenyatta alikariri kuwa Obama atakuwa mgeni wa serikali ya Kenya wala sio yeye kama rais Uhuru Kenyatta.
Aidha alisema ''swala la iwapo atakutana na naibu wa rais bwana William Ruto licha ya kukabiliwa na mashtaka katika mahakama ya ICC huko Hague halipaswi kuibuka''.
Huku hayo yakijiri, hali ya usalama imeimarishwa vilivyo katika mji wa Nairobi na viunga vyake na hasala maeneo yanayotarajiwa kuwa mwenyeji wa rais Obama.
Helikopta 4 za kijeshi za Marekani zilipaa juu ya mji wa Nairobi na kisha kutua katika chuo kikuu cha Kenyatta lililoko viungani mwa jiji hilo.

No comments:

Post a Comment