TANGAZO


Tuesday, July 21, 2015

Burundi:Uchaguzi wa urais umeanza

Uchaguzi wa urais umeanza Burundi
Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao.
Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.
Foleni zimeonekana katika vituo vya kupigia kura
Mwaandishi wa BBC aliyeko nchini humo anasema kuwa, milio ya risasi na gruneti imesikika usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura.
Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Raia wameanza kupiga kura Burundi
Viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Rais Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipiga foleni katika kituo kilichokaribu na mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura.
Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu
Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja wa Afrika katika muda wa lala salama.
Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa rais Nkurunziza.
Viongozi wanne wa upinzani wamesusia uchaguzi huo
Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Uchaguzi huu unafanyika licha ya taharuki kuhusiana na mgogoro wa kisiasa
Wagombea hao ni Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya.
Wapiga wanamchagua rais Burundi
Jina la rais Nkurunziza na ishara ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi.
Rais Nkurunziza ameonekana akipiga kura karibu na mji wa Ngozi
Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo.
Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Viongozi wa upinzani wamesusia kushiriki uchaguzi huo kwa dai rais anakuka sheria kwa kuwania muhula wa tatu
Kwa mujibu wa mshauri wa kisaisa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu
Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.

No comments:

Post a Comment