TANGAZO


Friday, June 26, 2015

Ziara ya Kinana Jimbo la Sumve, Mkoani Mwanza

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiswaga ng'ombe na mbuzi waliotoka kunywa maji kwenye lambo baada ya kuzindua katika Kijiji cha Kashilili wakati wa  ziara yake  Jimbo la Sumve, mkoani Mwanza, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. (Picha zote na Richard Mwaikenda; Kamanda wa Matukio Blog)
Komredi Kinana akizungumza wakati wa uzinduzi wa lambo hilo lenye maji safi na salama.
 
Komredi Kinana (katikati) na Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa (kulia) wakiangalia umeme wa jua unaosaidia kusukuma maji kwenda kwenye lambo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akizungumza na wananchi na kuwataka kulitunza lambo hilo.
Komredi Kinana akioneshwa chupa yenye mafuta ya alizeti alipokagua Mradi wa usindikaji wa alizeti katika Kijiji cha Lyoma, Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba leo.
Komredi Kinana akilakiwa kwa shangwe na nderemo nderemo katika Kijiji cha Malya na kutoa kilio cha cha kudhulumiwa viwanja vyao na Halamashauri ya Wilaya licha ya kulia fedha za kupimia.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, akijieleza mbele ya Komredi Kinana kuhusu dhuluma ya viwanja vya wanan Kijiji cha Malya.
Diwani wa Kijiji cha Malya akijeleza mbele ya Kinana kuhusu mggogoro wa viwanja katika kijiji hicho.
Komredi Kinana akipatiwa zawadi ya mafuta ya alizeti baada ya kukgaua kiwanda cha kusindika alizeti katika Kijiji cha Lyoma, Jimbo la Sumve.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akionesha kadi zilizorejeshwa na wananchama wa Chadema waliojiunga na CCM katika Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba, Mwanza.


No comments:

Post a Comment