Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakipata amaelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Steps Entertainment namna mtambo wakutengeneza DVD unavyofanya kazi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo akiangalia DVD ambayo imetengenezwa katika kiwanda cha Kampuniya Steps Entertainment jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi hiyo kutembelea wadau wa filamu nchini.Wa pili kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Filamu Dk. Vicensia Shule.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo akiangalia namna ya upakiaji wa DVD zinazotengenezwa katika kiwanda cha Kampuniya Steps Entertainment jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi hiyo kutembelea wadau wa filamu nchini.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakiangalia filamu ambayo imemaliza kutengenezwa muda si mrefu wakati wa ziara ya wajumbe hao katika kiwanda cha kampuni ya Steps kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Dilesh V. Solank akifafanua jambo wakati wa kikao na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea kiwanda cha kutengeneza Filamu kilichopo maeneo ya Kiwalani jijini Dar es Salaam jana. Kuliani Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Sylivester Sengerema.
Mjumbe wa bodi ya Filamu Tanzania Dk.Vicensia Shule akifafanua jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya Kiwanda cha Steps Intertainment (hawapopichani) mara baada ya kutembelea kiwanda cha kampuni hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mjumbe mwingine wa Bodi ya Filamu Bw. Bishop Hiluka.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Sylivester Sengerema (mwenye tai) na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo wakifuatilia hatua zautengenezaji wa DVD wakati wa ziara yao ya kutembelea wadau wa filamu jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Entertainment Bw. Jairaj Damodaran.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bw. Sylivester Sengerema, Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi.
Joyce Fissoo na Mkurugenzi Mkuu wa Steps Entertainment Bw. Dilesh V. Solank wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania
jana jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
No comments:
Post a Comment