Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Bw. Photi. A. Kagimbo akizungumza na ugeni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na ugeni kutoka Wizara ya Vijana na Uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe jana jijini Dar es Salaam kabla ya kutembelea SACCOSS ya vijana wa Temeke ili kujifunza masuala mbalimbali ya ujasiriamali kwa vijana. (Picha zote na Genofeva Matemu - Maelezo)
Baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Vijana na Uwezeshaji Uchumi kutoka nchini Zimbabwe wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Bw. Photi. A. Kagimbo (hayupo pichani) walipofika ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam na kupata taarifa ya maendeleo ya vikundi vya vijana wa Temeke wanaojishughulisha na masuala ya ujasiriamali.
Ofisa Maendeleo ya Vijana Manispaa ya Temeke Bibi Anna Marika (kushoto) akitoa historia fupi ya SACCOSS ya vijana wa Temeke jana jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ugeni uliotembelea SACCOSS hiyo kujifunza mambo mbalimbali. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa, wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa uwezeshaji uchumi kutoka Wizara ya Vijana na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Tafi Greemas Mashonganyika na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wizara ya Vijana, na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Emmanuel Ngwarati.
Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi Temeke Youth SACCOSS Bw. Maulidi Kulinga (aliyesimama) akitoa maelezo ya SACCOSS yao kwa ujumbe kutoka Wizara ya Vijana na Uwezeshaji Uchumi kutoka Zimbabwe walipowatembelea kujifunza jinsi wanavyoweza kusimamia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa (kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara ya ugeni kutoka nchini Zimbabwe waliofika nchini Tanzania kujifunza namna Serikali inavyoendesha na kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa uwezeshaji uchumi kutoka Wizara ya Vijana na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Tafi Greemas Mashonganyika na kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wizara ya Vijana, na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Emmanuel Ngwarati.
Baadhi ya wageni kutoka Wizara ya Vijana na Uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe wakiangalia usajili wa Temeke Vijana SACCOSS wakati wa ziara ya kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyoendesha na kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kulia ni Mwenyekiti wa SACCOSS hiyo Bw. Ismail Kassim.
Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Diana Kasonga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa ugeni kutoka nchini Zimbabwe walipotembelea kikundi cha vijana cha Waosha Magari Kibasili (WAMAKI) wakati wa ziara ya kujifunza jinsi Serikali ya Tanzania inavyoendesha na kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kushoto ni mmoja wa wanakikundi hicho.
No comments:
Post a Comment