Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
MAGONJWA yasiyo ya kuambukiza yakiwamo magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa kwa sasa huchangia zaidi ya asilimia hamsini ya matatizo yote yanatokana na maradhi duniani kwa njia ya ulemavu, vifo na gharama za matibabu hususan kwa kiasi kikubwa katika nchi zinazoendelea.
Tafiti mbali mbali zilizofanyika hapa Tanzania kwa watu wazima kati ya miaka ya themanini zimeonyesha uwepowa kisukari katika jamii kwa asilimia 1-3% na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5-10% huku viwango vya juu zaidi vikionekana katika jamii ya watu waishio mijini.
Mwaka 2012 tathminini iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50 ilionyesha kuwa viwango hivi viliongezeka hadi kufikia asilimia 9% kwa kisukari na asilimia 27% kwa msukumo wa juu wa damu. Ongezeko la viwango vilionekana pia katika lehemu , uzito na unene uliokithiri. Hali hii husababishwa na utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi yamwili, ulajiusiofaa, utumiaji wa tumbaku na pombe kupita kiasi
Mwaka 2011 mkutano Mkuu wa Viongozi wa Dunia katika Umoja wa Mataifa ulipitisha Azimio la Kisiasa kwa ajili ya kukinga na kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Kwa kuitikia mwito huo shirika la Afya Duniani (WHO) iliandaa mpango mkakati uliodhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa asilimia ishirini na tano (25%) ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza malengo ya hiari ili kufanikisha mkakati mzima. Malengo haya yaliridhiwa nanchi wanachama mwaka 2013 wakati wa Mkutano wa Afya Duniani (World Health Assembly) ikiwamo Tanzania.
Kila nchi mwanachama inatarajiwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ifikapo mwaka 2015 na pia kutoa taarifa ya utekelzaji wake ifikapo mwaka 2017.
Hata hivyo, Tanzania ilianza kushughulikia matatizo haya ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kuanzia mwaka 2009 kwa kuandaa mpango mkakati na mpago kazi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza wa mwaka 2009-2015 ambayo sasa unameisha muda wamwaka huu.
Mpango mkakati huu pia ulihusisha utekelazaji wa mpango wa Taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha ugonjwa wa kisukari Tanzania ambapo katika utekelzaji wake umegeuka na kuchukua dhana ya utekelezaji wa mpango wa taifa wa mangonjwa yasiyo yakuambukiza ambao huhusisha pia ufunguzi wa kliniki za magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika hospitali zote za mikoa na wilaya (ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75%), Elimu kwa watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya afya (ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 75%).
Sasa maandalizi yako katika kutoa elimu kwajamii ambapo wadau mbali mbali wanahusishwa kama jamii ya watu wa kansa (Tanzania Cancer Society), Umoja wa magonjwa ya moyo (Tanzania Heart Foundation) na umoja wa magonjwa sugu ya mfumo wa hewa (Tanzania Association of Respiratory Diseases).
Chama cha ugonjwa wa kisukari (Tanzania Diabetes Association) kwa kushirikiana na vyama hivi vingine vinaunda umoja wa magonjwa yayasiyo ya kuambukiza (Tanzania NCD Alliance, TANCDA). Vyama vyote hivi ni vyama vya wagonjwa lakini pia huwa na wataalamu wa afya pamoja na mtu awa yeyeyote mwenye masilahi na magonjwa haya.
Kwa kufanya kazi na kuongozwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na katika majukumu yao, TANCDA wamesaidia kufanikisha utayarishwaji wa rasimu ya mpango mkakati wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ya mwaka 2015-2020 ikihusisha pia vipaumbele tisa kama vilivyoainishwa na shirika la afya duniani (WHO) na pia mpango mkakati huu unalenga kuchukua nafasi ya mpango makakati unaoisha muda wake hivi karibuni.
Vipengele vingi katika mpango mkakati huu mpya unahusisha mipango kazi a mbayo ipo nje ya sekta ya afya na hivyo kuashiria uwepo wamahusiano madhubuti ya kisekta. Kwa hiyo nilazima sekta zote husika zishirikishwe mapema katika hatua za kimipango. Kwa vile mpango mkakati utahitaji rasilimali pesa nyingi na za kutosha nivyema ukahusisha wadau wote wa maendeleo, mashiirika ya Umoja wa Mataifa na hata wadau katika sekta binafsi.
Hivyo kutakuwa na Mkutano wa siku mbili kuanzia tarehe 1 hadi 2 mwezi wa saba utakaohusisha wadau wote utakaojadili kuhusu rasimu hi nahivyo kushirikisha wadau wote mapem a katika uchangiaji wa rasimu na kuleta hali ya umilikaji wa mpango mkakati mzima wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kujenga ufahamu wa wadau hawa muhimu juu ya matatizo yatokanayo na magonjwa yasiyo yakuambukiza.
Matarajio ya mkutano ni kama yafuatayo:
Kujenga ufahamu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa wadau wote.
Kuwa na viashiria vya gharama ya utekelezaji wa mpango mkakati na mpango kazi mzima.
Ukubalikaji wa rasimu ya mpango mkakati na mpango kazi kwa wadau wote.
Kukubaliana juu ya mapendekezo na jinsi ya kufanikisha utekelezaji wa mpango mkakati ikiwa ni pamoja na mpago kazi.
No comments:
Post a Comment