Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe akizungumza alipokuwa akiwakaribisha wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Wizara wa Fedha kwenye ufunguzi wa kikao cha kikao cha baraza hilo lililofanyika leo mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Fedha ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile akitoa neno kabla ya ufunguzi wa kikao cha baraza hilo lililofanyika leo mjini Morogoro.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya Fedha lililofanyika leo mjini Morogoro. (Picha zote na Wizara ya Fedha)
Na Mwandishi wetu
03/06/2015
WAAJIRI na wafanyakazi wameaswa kutumia fursa ya kukutana mara kwa mara ili kujadiliana masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayohusu maendeleo ya watumishi, kuongeza na kuimarisha bidii na utendaji wa kazi kulingana na sheria, kanuni na taratibu na kufikia azma ya nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya alipokuwa akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la wizara hiyo leo mjini Morogoro.
Waziri Saada alibainisha kuwa lengo la kikao cha baraza hilo lilikuwa ni pamoja na kujadili na kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2014/2015 na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Fedha kwa mwaka 2015/2016 kabla ya kupitishwa Bungeni.
“Ili kuwa na mabaraza yenye tija mahali pa kazi, mabaraza ya wafanyakazi yanawajibu wa kuimarisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uendeshaji wa shughuli za taasisi na hivyo kuwa na uongozi wa pamoja” alisema Waziri Saada.
Akisisitiza kauli ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete anayoituimia mara kwa mara, Waziri Saada amesema kuwa “Hazina ni moyo wa Serikali” na kuwaasa wafanyakazi wa Wizara hiyo watumie vema rasilimali rasilimali zilizomo, zinazokusanywa na zile za wahisani na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali.
Aidha, Waziri Saada amewahimiza wajumbe hao wa kikao kutoka kutoka mikoa mbalimbali nchini kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu nchini ambapo wajumbe wamekumbushwa kutumia fursa waliyonayo na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura nchini ili waweze kuchagua viongozi watakaosaidia kusukuma maendeleo mbele maendeleo ya nchi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe alisema kuwa mkoa wa Morogoro ni salama na ni mahali pazuri pa kuishi ikizingatiwa kuwa na hali nzuri ya kiulinzi na usalama mkoa mzima.
Mkuu huyo wa mkoa Dkt. Rutengwe aliwahakikishia wajumbe wa kikao hicho kuwa mkoa huo unahali nzuri ya usafi wa mazingira ukipambwa na safu za milima ya Uluguru ambazo zinaendelea kuhifadhiwa kwa hali ya juu ili kuendelea kuwa ni kivutio cha watu wengi wa nadani na nje ya nchi kuja Morogoro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa baraza hilo liliwahusisha wakuu wa idara mbalimbali ndani ya wizara ambalo linashirikisha wafanyakazi wote katika kuandaa bajeti yao na hivyo kuwa na bajeti shirikishi.
No comments:
Post a Comment