TANGAZO


Wednesday, June 3, 2015

Msanii Q Chilla kuzindua kazi zake mpya za filamu na nyimbo keshokutwa Mbezi jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kampuni ya Q Mhonda, Joseph Mhonda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu udhamini wake kwa msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila' (kulia), katika uzinduzi wa kazi zake mpya, zikiwemo za filamu na nyimbo, utakaofanyika keshokutwa, Mbezi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii Mohamed Ally 'MB Dog'. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila', akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa kazi zake mpya, zikiwemo za filamu na nyimbo, utakaofanyika keshokutwa, Mbezi jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdhamini wake, Mkurugenzi wa Q Mhonda, Joseph Mhonda na kushoto ni msanii mwenzake, Mohamed Ally 'MB Dog'.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila', alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa kazi zake mpya, zikiwemo za filamu na nyimbo, utakaofanyika keshokutwa, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila', akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa kazi zake mpya, zikiwemo za filamu na nyimbo, utakaofanyika keshokutwa, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Msanii Mohamed Ally 'MB Dog', akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Kulia ni mdhamini wake, Mkurugenzi wa Q Mhonda, Joseph Mhonda.
Msanii Mohamed Ally 'MB Dog', akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Katikati ni mdhamini wake, Mkurugenzi wa Q Mhonda, Joseph Mhonda na kulia ni msanii mwenzake,  Aboubakar Katwila 'Q Chila'.
Msanii Mohamed Ally 'MB Dog', akighani moja ya wimbo wake mbele ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo.
Msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila', akighani moja ya wimbo wake mbele ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni mdhamini wake, Mkurugenzi wa Q Mhonda, Joseph Mhonda.
Msanii Aboubakar Katwila 'Q Chila', akighani wimbo wake mbele ya waandishi wa habari jijini leo, huku mdhamini wake, Mkurugenzi wa Q Mhonda, Joseph Mhonda (kushoto), akimuangalia.
Msanii Uwesu Ramadhan, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni msanii mwenzake, Aboubakar Katwila 'Q Chila'.
Msanii Uwesu Ramadhan, akighani moja ya nyimbo zake katika mkutano huo. Kushoto ni msanii mwenzake, Aboubakar Katwila 'Q Chila'.

No comments:

Post a Comment