TANGAZO


Wednesday, June 3, 2015

Waandaaji wa Tamasha la Bagamoyo Historical Marathon wazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Mratibu wa mbio za Bagamoyo Historical Marathon 2015, zilizoandaliwa na Kampuni ya 4Bell, Dorah Raymond akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mbio hizo zitakazofanyika Juni 14, mwaka huu, Bagamoyo mkoani Pwani. Kulia ni Mratibu Fatma Hamis. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mratibu wa mbio za Bagamoyo Historical Marathon 2015, zilizoandaliwa na Kampuni ya 4Bell, Dorah Raymond akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akijibu maswali kuhusu mbio hizo, zitakazofanyika Juni 14, mwaka huu, Bagamoyo mkoani Pwani. Kulia ni Mratibu Fatma Hamis.

TAARIFA FUPI KUHUSU BAGAMOYO MARATHON
Ndugu waandishi wa habari,
UTANGULIZI 
Leo tumefika hapa kuutaarifu umma kuwa Tamasha la Bagamoyo Historical Marathon litafanyika kwa mara ya pili siku ya Jumapili, tarehe 14 Juni  2015 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Ndugu waandishi wa habari, Tamasha la Bagamoyo Historical Marathon lilifanyika kwa mara ya kwanza na kwa mafanikio mjini Bagamoyo tarehe 22 Juni 2014 ambapo lilihudhuriwa na takriban watu 1000. Tunawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya mafanikio yale. Karibuni tena na tunaomba ushirikiano wenu kufanikisha na hili pia.

Maudhui yetu mwaka huu ni “ANZA KUKIMBIA, UJIKINGE NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA” yaani “PREVENT NON-COMMUNICABLE DISEASES, START RUNNING”.  Hivyo uzinduzi wa mwaka huu ulifanywa na Mwakilishi wa Waziri wa Afya tarehe 19 Machi 2015 mjini Bagamoyo. Pia uzinduzi ulipata uwakilishi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo na pia Chama cha Riadha Tanzania. 

Nia na Madhumuni:

KUHAMASISHA AFYA BORA– kutokana na ongezeko kubwa la matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ambukizwa (Non-Communicable Diseases-NCDs) , Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbali mbali inasisitiza mazoezi hasa kutembea, mchaka-mchaka (jogging) na kukimbia kama njia kuu ya kudumisha afya na kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, shinikizo la damu n.k. Mbio hizi zitahamasisha ufanyaji wa mazoezi hasa yale ya kukimbia na hivyo kusaidia kupunguza matukio na vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza.

KUKUZA UTALII – kama inavyofahamika Bagamoyo ndiyo mji mkongwe kuliko miji yote nchini Tanzania ambao umepitishwa na UNESCO kuwa eneo la saba lenye uhifadhi wa historia ya kale (Seventh World Heritage Site). Mji huu   ulikuwa moja ya soko kuu la watumwa katika Afrika mashariki na kati, hivyo mbio hizi zitasaidia kuutangaza, kuhamasisha na kukuza utalii katika mji huu muhimu kihistoria nchini na hivyo kuchangia kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.


KUCHANGIA MAENDELEO KIUCHUMI – kwa kuwa matarajio yetu ni kuwa na wageni wengi kwa tukio hili katika mji wa Bagamoyo tunatumaini kuwa tukio hili litaongeza shughuli za kibiashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo hivyo kuboresha uchumi wa mji huu.

KUENDELEZA RIADHA TANZANIA

Na nia ya mwisho, japo ndio kuu hasa, ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji vya mbio ndefu na baadaye kujenga kambi itakayowawezesha kuwajenga kinidhamu ili waweze kushiriki na kushinda mbio ndefu maarufu duniani siku za usoni. Tunaamini katika maandalizi sahihi ya washiriki ili kurejesha vyema heshima ya Tanzania katika mchezo wa riadha.

Mbio hizi zinatarajia kushirikisha makundi ya mbali mbali ya watu kama ifuatavyo:-

Wakimbiaji wataaluma (professional athletes) 
Kilomita 21.1 Umri wa miaka 14 na kuendelea.
Wakimbiaji wengine (casual runners)
KM 10  Umri wa miaka 14 na kuendelea
KM 5    Family Fun Run. 

Tamasha hili litajumuisha mbio zifuatazo:-

Mbio ndefu za 21.1 km (Half Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:30 asubuhi (6:30AM sharp) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia (Mangesani Road) na baadaye, kupitia Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam na kugeuzia maeneo ya Kiromo.

Mbio ndefu za 10.5 km (Quarter Marathon) - Mbio hizi zinaratajiwa kuanza saa 12:45 asubuhi (6:45AM) ambapo zitaanzia Uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road, katikati ya mji na kisha kuchukua Bagamoyo Road uelekeo wa Dar es Salaam mpaka makutano ya Barabara ya Msata. 


Kisha watachukua uelekeo wa kuelekea Msata takribani kilomita nne (4)  ambapo watageuza kurejea uwanja wa shule ya Mbaruku.


Mbio za kujifurahisha (Fun Run) - Mbio hizi zinatarajiwa kuanza saa 01:00 pale uwanja wa Shule ya Msingi Mbaruku kupitia Mangesani Road na  kuelekea upande wa mahoteli ya kitalii mpaka kufika kituo cha zimamoto  ambapo washiriki watageuza kurudi uwanja wa Mbaruku. 


BURUDANI

Hii ni nafasi nzuri sana kwa wale watakaweza kufika Bagamoyo siku moja kabla (Jumamosi ya tarehe 13 Juni) na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria Bagamoyo, kama, Kaole ruins, Kanisa la Mwanzo Africa Mashariki, nk.
Weekend gateaway.

Bagamoyo kuna hotel nzuri sana za ufukweni, hivo tunawahimiza hasa watu wa Dar es salaam kufika na ku ‘refresh’ baada ya shughuli za kila siku kwenye jiji letu hili la Dar es salaam. Tungependa sehemu kubwa ya jiji ihamie Bagamoyo wikiendi ya tarehe 14. Mazungumzo yanaendelea na hotel mbali mbali za Bagamoyo ili kupata malazi kwa bei za punguzo. 


UANDIKISHWAJI

Ndugu waandishi wa Habari ,
Uandikishwaji utaanza rasmi siku ya Alhamis tarehe 04 Juni  2014, katika maeneo  yafuatayo:- 

Tunatarajia kuwa na Vituo mbalimbali jijini na kwa kuanzia tutakuwa Quality Centre, Msasani Mall , KIBO Complex na Mlimani City,kwa kuanzia. Vituo vingine tutaendelea kufahamishana kadiri tunavyovipata. Kila mshiriki atakapo jiandikisha atapata T-shirt.


ZAWADI

Ndugu Waandishi wa Habari, Tunatarajia kuwa na zawadi nono na kwa washiriki wengi, kama ifuatavyo licha ya  washindi 200 wa Mwanzo kwa Half Marathon kupata Nishani (Medal) .

  21.1 km Half Marathon 10.5 km Half Marathon   
  Gents Ladies Gents Ladies   
Mshindi 1             500,000          500,000         100,000         100,000   
Mshindi 2             400,000          400,000           80,000           80,000   
Mshindi 3             300,000          300,000           50,000           50,000   
Mshindi 4             200,000          200,000           40,000           40,000   
Mshindi 5             150,000          150,000           40,000           40,000   
Mshindi 6             100,000          100,000           40,000           40,000   
Mshindi 7               80,000            80,000           40,000           40,000   
Mshindi 8               50,000            50,000           40,000           40,000   
Mshindi 9               50,000            50,000           40,000           40,000   
Mshindi 10               50,000            50,000           40,000           40,000   
  1,880,000 1,880,000 510,000 510,000  

SHUKRANI 
Tunashuruku kwa ushirikiano uliotolewa na Ofisi ya Mkoa wa Pwani, Ofisi ya Wilaya ya Bagamoyo na pia Chama cha Riadha Tanzania na tunaendelea kuomba ushirikiano Zaidi ili kufanikisha mbio hizi. Pia tunawashukuru wadhamini ambao wameshajitokeza kutudhamini hadi sasa Coca cola, NHIF, Azam Media, E-FM, MILES, Synchro Site Watch, Spheres Insurance, Softnet.  Maelezo zaidi yanapatika kwenye website yetu www.bagamoyomarathon.co.tz

Tuungane kupiga na Magonjwa yasiyoambukizwa na pia kuitangaza Bagamoyo Yetu.

Karibuni sana Bagamoyo.
Dominic Mosha 
Mratibu 

No comments:

Post a Comment