Mwenyekiti wa Vuguvugu la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumawata), Ally Makwiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitangaza kuhusu umoja huo, kumuunga mkono mtangaza nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa katika nia yake ya kuwania Urais wa Muungano. Katikati ni Mweka hazina wa Vumawata, Perice Makau na kulia ni mjumbe wa umoja huo, Muhibu Mustafa. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Vuguvugu la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumawata), Ally Makwiro, alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu umoja huo, kumuunga mkono mtangaza nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa katika nia yake ya kuwania Urais wa Muungano.
Mwenyekiti wa Vuguvugu la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumawata), Ally Makwiro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kumuunga mkono, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa katika azma yake ya kuwania nafasi ya Urais.
Mwenyekiti wa Vuguvugu la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumawata), Ally Makwiro (kulia), alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (kushoto), Dar es Salaam leo.
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Vuguvugu Maalumu la Mabadiliko ya Walimu Tanzania (Vumawata), wenye walimu 101,206 umeamua kumpigia debe mgombea urais Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kwa kuona kuwa anaweza kutatua changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na kupigania maslahi yao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya walimu wa umoja huo, Mwenyekiti wa Vumawata Taifa, Ally Makwiro alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na walimu wengi kunyimwa maslahi yao ya msingi na kwamba lengo lao ni kuona walimu wanachagua kiongozi halali ambaye atatatua changamoto walizonazo.
Alisema wameona kuwa Lowassa anafaa kutokana na kuacha alama ya kumbukumbu kwa vizazi na vizazi vya watanzania wanyonge wa kipato cha chini kutokana na kusimamia kwa nguvu na kuhakikisha kila kata nchini inakua na shule ya sekondari.
Aliongeza kuwa Lowassa ni mgombea aliyeonesha nia kwa kuipa elimu kipaumbele kwa kusema Elimu kwanza ambapo walimu wanaamini kuwa endapo atakuwa Rais uhakika wa maslahi ya walimu utabadilika kwa haraka.
Aidha alisema kuwa mgombea huyo alikua akishiriki katika mambo mablimbali ya kutatua changamoto za walimu ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye harambee mashuleni.
Makwiro alisema ndapo Lowassa atakuwa kiongozi ataweza kutatua changamoto za Posho kwa walimu ambapo ndio chanzo cha kuonekana mishahara midogo na kwamba haitoshi.
Alisema nyumba za walimu pia ni changamoto ambayo husababisha kilio kwa walimu kwa muda mrefu ambapo walimu wanaishi maeneo ya mbali na wanapofundisha.
Mwenyekiti Makwiro alisema upandishwaji wa mishahara ya walimu unahitajika kuboreshwa ili iendane na kazi wanazofanya hivyo wameamua kumpigia debe ili atatue changamoto hizo.
Hata hivyo aliongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na kuanzishwa kwa maduka maalum ya walimu, malipo ya madeni ya walimu kwwa wakati,upandishaji wa hadhi ya walimu pamoja na uboreshaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment