TANGAZO


Wednesday, June 3, 2015

Shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Dar es Salaam

 
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue
(kulia) akisalimiana na Waziri wa Fedha wa zamani
na Mbunge wa Kilosa Mhe. MustafaMkulo alipowasili 
kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kwa 
ajili ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen 
Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga jijini 
Dar es Salaam.   
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu 
(kulia) akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job 
Ndugai leomjini Dodoma kwenye shughuli ya kuaga 
mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa
Mbunge wa Ukonga jijini  Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue 
akisaini kitabu cha wageni waliofika kwenye shughuli 
ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa
aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika
viwanja vya Bunge mjini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe.
Anna Abdallah akimfariji mume wa marehemu Mhe. 
Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku
wa kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma. 


Waheshimiwa Wabunge na baadhi ya watu mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga.
Mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa. 

Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi
mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu  
Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga
kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma wakati wa  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa. 
Kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoa salam za bunge kwenye  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma. 
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa maombolezo kwenye  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma. 
Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa  marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma. 
Baadhi ya wabunge wakitoa pole kwa wanafamilia wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma. 
Mchungaji Mshana Samweli wa KKKT Jimbo la Dodoma akitoa neno kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa leo mjini Dodoma. (Picha zote na Fatma Salum-Maelezo)

No comments:

Post a Comment