TANGAZO


Monday, June 29, 2015

Wanafunzi wavutiwa na maonesho ya ALAT

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sabodo kidato cha nne wakitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea maonesho ya Serikali za Mitaa (ALAT), yanayofanyika katika Uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sabodo kidato cha nne wakitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea maonesho ya Serikali za Mitaa (ALAT), yanayofanyika katika Uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara. 

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Rahaleo wakijifunza kwakutumia kompyuta masomo mbalimbali, ikiwemo Hesabu katika maonesho ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Na mwandishi wetu
KUFATIA Mkoa wa Mtwara kuwa wenyeji wa maonesho ya Serikali za Mitaa banda la Wilaya ya Mtwara limekuwa likivutia vijana wengi kutokana na kuweka vifaa vya elimu ambayo vinawafanya wajifunze zaidi.

Maonesho hayo yatakayodumu kwa siku saba sambamba na elimu mbalimbali kutolewa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sabodo wamepata nafasi ya kujifunza na kutoa elimu kwa tu malimbali kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi.

Wanafunzi hao ambao wanatumia maabara inayohamishika ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wa shule zingine kuhamasika katika kujifunza na kuyapenda masomo yasayansi ambayo kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiyaogopa.

Editha Masia mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mustapha sabodo anasema kuwa katika masomo ya sayansi amekutana na changamoto nyingi ambazo zimeweza kumsaidia kujifunza zaidi.

Anasema kuwa uwepo wa masomo hayo unatoa nafasi kwa wanafunzi kujifunza ili waweze kuwa wataalam wa baadae sio kuyakimbia hali ambayo inapelekea madktari na walimu kupungua kwa kiasi kikubwa.

“Masomo haya ni mazuri endapo mwanafunzi atajifunza kwa vitendo unajua hiki kigololi nilichoshika bila sayansi kinaweza kupitiliza katika hili lingi lakinikwakutumia sayansi naweza kulikuza ikashindwa kupita hapa katika hili tundu”  alisema Masia

Nae Issa Juma mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mustapha sabodo anasema kuwa wazazi wanapaswa kuhamasisha watoto wao kujifunza masomo ya sayansi ili waweze kujifunza mengi ambayo yanaweza kuwasaidia katika siku zijazo.

Anasema kuwa uoga wa kuchukua masomo ya sayansi ni sababu ya wanafunzi hao kuogopa kuyasoma hivyo kuambukizana ili hali masomo hayo yanaonyesha upendeleo hasa unapofika katika ngazi ya elimu ya juu.

“Sayansi inatoa madaktari, wanasayansi, walimu na kada zingine nyingi lazima tutumie njia za makusudi ili kuweza kuhamasisha wanafunzi wengi kukimbilia masomo hayo muhimu kwa dunia ya sasa” alisema Juma

Kwa upande wa shule za msingi katika banda la maonyesho la mtwra mikindani hawakuwaacha wanafuzi wa shule za misingi ambao kwa sasa wako likizo kwa kuwawekea komputa na jinsi ya kujifunza kwa lugha za alama ambazo zinasaidia watu wenye ulemavu kuelewa zaidi.

Wanafunzi hao walionyesha ustadi wa kutumia komputa hizo za kujifunzia ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kuhamasisha wanafunzi kudhuria masomo kwa wakati na kupunguza utoro kwa wanafunzi wa madarasa ya chini la kwanza na darasa la pili.

Kwa upande wa halmashauri ya mji wa masasi wamelalamikia ukosefu  wa vipimo katika shule za watoto wenye mahitaji maalumu umepunguza idadi ya uandikishwaji watoto wenye umri wa kwenda shule kwa lengo la kufanikisha Mapango wa Matokea Makubwa sasa (BRN).

Nae  Afisa Elimu Maalum wa Halmashuri ya Masasi Mkoani Mtwara, Adrew Magani akitoa maelekezo kwa wananchi katika Maonyesho ya Serikali za Mitaa (alat) katika viwanja vya Mashujaa Mjini hapa anasisitiza wazazi wenye watoto wenye ulemavu kupeleka watoto wao shuleni na kuacha tabia ya kuwaficha majumbani.

Hata hivyo anaongeza kuwa endapo wazazi watapata mwamko zoezi hilo la undikishaji linaweza kufikia malengo ya BRN  kama kituo cha watoto wa mahitaji maalum kitakuwa kinafanyakazi yake ipasavyo.

Magani anasisitiza kuwa kutokana na hilo Halmashari hiyo baada ya kuona umuhimu wa kituo hicho cha upimaji wakaamu kuleta kituo hicho katika Maenesho hayo ili watanzania  waweze kujifunza hasa wa mkoani hapa jinsi ya kuwasidia watoto wenye mahitaji maalum.

Aidha Afisa huyo anasema kuwa maonyesho hayo yana umuhimu mkubwa kutokana na kuwafundisha watu mbalimbali jinsi ya kuwasaidia watoto hao ili waliowaficha waweze kuwafichua na kuwapeleka shuleni.

“ Maonyesho haya ni muhimu sana… kwetu  kwa sababu tunawaelekeza jamii kuona jinsi gani tunaweza kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalum ili wale ambao wamewafisha waweze kuwafichua na kuwapeka shuleni ndio maana tunawaonyesha jinsi tunavyoweza kuwahudumia.” Alisema Magani

Hata hivyo aliongeza kuwa watoto wenye mahitaji maalum wanaweza kuchanganyika katika Darasa Moja na watoto wengine  kulingana na uelewa wao ili kutimiza ile Lengo la Elimu Jumuishi linaweza kukamilika.

“Walemavu ni wengi lakini hawapati nafasi ya kupata kile ambacho wengine wanakipata wakiwa shuleni ndio maana tunahamasisha wazazi kuwatoa ndani watoto waliowafungia ili waweze kupata haki zao za msingi……

“Hawa watoto wanapaswa kujifunza lakini wazazi wengi wanaficha hawawa peleki shuleni  hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu hakuna mtoto ambae hawezekani wote wanafundishwa na wakaelewa kulingana na uwelewa wao na wanaweza wakachanganyika na watoto wengine katika darasa moja na ile lengo la elimu jumuishi linaweza kukamilika” alisema Magani.

No comments:

Post a Comment