TANGAZO


Monday, June 29, 2015

Vijana 500 waitimu mafunzo ya ujasiriamali pamoja na elimu ya kiroho


Waumini wakiwa katika kanisa la PEFA jana kwenye hitimisho la kongamano la vijana ambalo limefanyika kwa takribani siku saba. (Picha zote na Frankius Cleophace)
Waumini wakiwa katika kanisa la PEFA jana kwenye hitimisho la kongamano la vijana ambalo limefanyika kwa takribani siku saba.
 
Na Frankius Cleophace Tarime.
KANISA la Pentecostal Evangelistc Fellowship Of Afrika lililopo Mji mdogo wa Sirari mpakani mwa nchi za Tanzania na Kenya, wilayani Tarime, mkoani Mara, wametoa mafunzo ya Ujasiliamali  kwa vijana zaidi ya miatano kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuondokana na utegemezi huku wakifundishwa uhaminifu katika maisha yao jamba ambalo litatumika kumutukuza mwenyezi mungu na kubadili mienendo na tabia za vijana hao.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi, Mchungaji Stive Mhechi ambaye pia alikuwa mmoja kati ya Walimu walikuwa wakitoa mafunzo kanisani hapo alisema kuwa kanisa limeamua kukutanisha vijana hao  kutoka makanisa yote ya Pefa yaliyomo ndani ya wilaya ya Tarime kwa lengo la kuwajengea uwezo mkubwa ili waweze kuondokana na utegemezi huku wakisudia kumutumikia mwenyezi Mungu.

Aidha Mchungaji huyo alisema kuwa vijana hao wameweza kufundishwa mada uhaminifu katika suala la bihashara na wale ambao wameoa wamefundishwa uhaminifu katika ndoa.

“Tumekuwa tukiona Ndoa za watu wengi zinaharibika kwa sababu ya ukosefu wa uhaminifu hivyo kupitia mafunzo haya itasaidia kubadili mienendo na tabia za vijana wetu ambao tumeendelea kuwaea kiroho na kimwili” alisema Mchungaji

Mafunzo hayo yamefanyika kanisani hapo takribani wiki moja kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana hao ili waweze kuondokana na utegemezi ususani vijana wanaoisha maeneo ya mipakani wamekuwa wakitegemea ajira kutoka serikalini hivyo kupitia mafunzo hayo vijana hao wataweza kkujishughulisha.

Kwa upande wake mwenyekiti wa vijana Kanisa la Pefa Wilayani hapa Barnanabas Mchuma alimetumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuzidi kusikiliza kilio cha vijana ili waweze kuondokana na utegemezi.
 
“Sisi kama kanisa tumeweza kutoa mafunzo haya ya ujasiliamali pamja na mafunzo ya kiroho hivyo serikali nao awewze kutuunga mkono ili kuweza kukomboa vija na kukuza uchumi wa Taifa”alisema Mchuma.

Aliongeza kuwa ukizingatia Mji mdogo wa sirari uko mpakani mwa nchi jirani ya Kenya na Tanzania hivyo vijana hao wakipta fursa  wataweza kuzitumia ipasavyoo kwa lengo la kujiongezeakipato.

No comments:

Post a Comment