TANGAZO


Monday, June 1, 2015

Profesa Mwandosya atangaza nia ya kugombea Urais wa Muungano

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Mbeya, wakiongoza maandamano ya kumpokea Profesa Mwandosya wakiwa na bango kubwa kuelekea eneo la viwanja vya mkutano katika ukumbi wa Mkapa Sokomatola jijini Mbeya leo.
Profesa Mwandosya akielekea kwenye eneo la mkutano ambako alikuwa akienda kutangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi ujao. 
Profesa Mwandosya pamoja na viongozi wengine wakiwa jukwaa kuu kabla ya kutangaza nia rasmi ya kugombea Uarais katika Uchaguzi Mkuu ujao. 
Viongozi wa dini na kimila wakiwa eneo la mkutano kumsindikiza Profesa Mwandosya akitangaza nia ya kugombea urais. 
Wananchi na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakitoa fedha za kumsaidia Profesa Mwandosya kuchukua fomu ya kugombea urais ambazo zilipatikana shilingi Milion 10.7. 
Mwenyekiti wa Mujata, Chifu Soja Shayo akisalimiana na Profesa Mwandosya kama ishara ya kumpa baraka kuelekea kuchukua fomu ya kugombea urais. 
Profesa Mark Mwandosya akizungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani waliojitokeza kumsikiliza akitangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM. (Picha zote na Venance Matinya)

No comments:

Post a Comment