Mtoto wa Muasisi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, Balozi Ali Karume, akiwa katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati, uliopo Dunga kisiwani Unguja leo. (Picha zote na Haroub Hussein).
Waalikwa mbali mbali wakiwa katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi ulioitishwa na Balozi Ali Karume katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kati, Hassan Mrisho akimkaribisha Balozi Ali Karume kuhutubia katika mkutano wake wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Balozi Ali Karume alitangaza nia yake katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga.
Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati uliopo Dunga.
Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati uliopo Dunga.
Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati uliopo Dunga.
Balozi Ali Karume akizungumza katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati uliopo Dunga.
Waalikwa mbali mbali wakiwa katika mkutano wa kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi ulioitishwa na Balozi Ali Karume katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga.
....Naye Makongoro Nyerere atangaza nia
*Asema yeye hawezi kusema atawafanyia nini watanzania bila kuiona ilani mpya kwani bado haijapitishwa
*Asema Rais Kikwete ni mzuri ila wanaomuangusha ni rafiki zake
Charles Makongoro NyerereMakongoro Nyerere, akizungumza wakati alipokuwa akitangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano, nyumbani kwao, Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo.
Makongoro Nyerere, akivishwa mgolole wa Kabila lake la Wazanaki na wazee wa kabila hilo, wakati alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano, nyumbani kwao, Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo.(Picha zote na Mashaka Baltazar)
Na Ahmewd Makongo, Butiama
Juni 1, 2015.
MTOTO wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Charles Makongoro Nyerere, leo ametangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapiunduzi (CCM), akiwa nyumbani kwao Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Akitangaza nia hiyo mbele ya umati mkubwa wa wananchi waliofika katika eneo hilo, Makongoro Nyerere, alisema kuwa yeye hawezi kusema kwamba atawafanyia nini wananchi wakati Ilani ya chama hicho bado haijapitishwa na vikao halali vya chama hicho.
Alisema kuwa Ilani ya chama hicho ndiyo inayoongoza kila kitu, ambapo mgombea yoyote wakati anajinadi atakuwa anatoa ahadi zake kutokana na maelekezo yaliyomo ndani ya Ilani hiyo.
Hata hivyo Makongoro aliwashangaa wanachama wenzake ambao tayari wamekwisha tangaza nia ya kuwania nafasi hiyo na kutoa ahadi nyingi, wakati Ilani hiyo haijapitishwa kwa sababu CCM inaongozwa kwa vikao na kufuata katiba na taratibu zake.
Alisema Ilani hiyo itapitishwa mwezi wa saba lakini waliotangaza nia akiwemo mwenyekiti wa kuandaa ilani hiyo, ambaye pia ni Waziri wa kilimo, chakula na ushirika Stephen Wassira, wao tayari wamekwishatoa ahadi kibao, bila kuwa na Ilani.
Alisema kuwa yeye kamwe hawezi kuwaambia wananchi kwamba atawafanyia nini wakati hajaiona Ilani hiyo ambayo ndiyo msingi wa wagombea wote wa CCM.
“Mimi hapa siwezi kabisa kusema nitawafanyia nini wa Tanzania, bila kuwa na Ilani ya chama, maana naweza kusema nitafanya hiki lakini kwenye Ilani ya chama jambo hilo halimo” alisema na kushangiliwa na umati mkubvwa wa watu.
“Ilani bado haijatoka ambayo inazungumzia mambo yote ambayo mgombea wa CCM, naye atayazungumzia…….chama chetu kina utaratibu wake mzuri tu….” alisema.
Aidha, akizungumzia kilichomfanya akihame chama hicho na kuhamia NCCR-Mageuzi, kwamba ni kutokana na kushauriwa na waasisi wa CCM, wakati akigombea ubunge katika jimbo la Arusha kipindi hicho.
Alisema kuwa waasisi hao walimshauri afanye hivyo baada ya kufanyiwa mizengwe ya kutaka kutopitisha jina lake kwenye vikao vya chama hicho kutokana na kutokuwa na fedha za kutoa rushwa, na kwamba kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi alimuona mzazi wake mwalimu Nyerere ambaye alimkubalia na kumpatia Baraka zote.
“Mimi na mke wangu tulimfuata mwalimu Nyerere na nikamwambia jinsi ninavyotaka kukihama chama hicho na jinsi nilivyoshauriwa na waasisis hao, alinikubalia na kunipa Baraka zote”.
Alisema kuwa baadaye alimua kurejea CCM na kuongeza kuwa CCM ni chama kizuri chenye katiba nzuri na utaratibu wake ni mzuri, lakinio katiba hiyo pamoja na taratibu zake imekuwa ikikiukwa kwa makusudi na baadhi ya wanachama ambao wengi wao ni matajiri wanaotumia fedha zao kukigawa chama hicho.
Alisema matajiri hao fedha zao nyingi ni chafu na wamezichota serikalini wakiwa katika chama hicho na kwamba yeye hakatai watu kuwa matajiri lakini wawe na utajari ambao ni halali.
Aliongeza kuwa viongozi hao ambao baadhi yao tayari wamekwishatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu nchini, wamekwisha kigawa chama chao.
Alisema kuwa na sasa CCM imefikia hatua mbaya sana kwa sababu mgombea akiwa hana fedha za kutoa rushwa hawezi kuchaguliwa, na kwamba yeye anaamini kutokana na uadilifu wake alionao atachaguliwa na Watanzania kwa sababu wananchi wanaopinga mambo hayo ni wengimno na watamuunga mkono.
Alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wanaotoa rushwa ambayo amedai inamchukiza sana kisha kuwagawa wanaCCM, ni bola wakatoka kwenye chama hicho, kwani hicho chama ni mali ya wananchi na siyo mali yao kama wanavyodhania.
“Watoke watuaachie chama chetu, wanataka kukipeleka wapi watoke watuaachie chama chetu” alisema.
Aliongeza kuwa akiteuliwa na chama hicho na kisha kuchaguliwa kuwa Rais, pamoja na kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa, atahakikisha chama hicho kinarudi kwenye misingi yake aliyoiacha baba wa Taifa mwalimu Nyerere.
Alisema kuwa atawabana wabadilifu wote wa mali za umma ambao wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya, kwani wanakiuka misingi ya chama hicho kwa makusudi na amewaita viongozi hao kuwa ni vibaka.
“CCM kuna vibaka wetu na Vyama vya upinzani nao wana vibaka wao, watoke watuaachie chama chetu” aliongeza.
Alisema kuwa yeye pamoja na kutokuwa na pesa za kutoa rushwa na pia siyo mtoa rushwa, au kuwa na makundi kama walivyo wengine anaamini kwamba atapatiwa nafasi hiyo kwa sababu anazo sifa za kutosha na pia ni muadilifu na anafuata misingi ya katiba ya chama hicho.
Alisema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni mtu safi ila wanaomuangusha tena kwa makusudi na kumdhalilisha mbele ya jamii ni baadhi ya marafiki zake, kwa sababu ya kuwaonea huruma.
Aidha, alisema kuwa Rais Kikwete anaijali sana familia ya Mwalimu Nyerere.
Alisema kuwa pia anasikitishwa sana na kitendo cha wanajeshi, polisi na mahakimu kulipwa mshahara mdogo wakati kazi wanayoifanya ya kutumikia taifa ni kubwa na ngumu.
Alisema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu pia wamekuwa wakiandamana na kupigwa mabomu wakati wakidai mikopo yao ambayo ni haki zao kimsingi, wakati serikali inazofedha nyingi tu lakini haijali hilo jambo.
Kabla ya kutangaza nia yake wazee wa Kabila la Wazanaki wakiongozwa na Chifu Wanzagi walisema imefika hatua sasa Mwalimu Nyerere atambuliwe na kukumbukwa kwa kuenziwa kwa mtoto wake kupewa nafasi hiyo ya Urais kama walivyo marais wengine, akiwemo Karume na Kenyata wa Kenya.
Aidha, mkutano huo ulitanguliwa na maombi ya sala na dua kutoika kwa viongozi wa madhehebu ya dini wakimuombea Makongoro Nyerere apewe nafasi hiyo ya urais.
No comments:
Post a Comment