TANGAZO

Friday, June 5, 2015

NEMC yasema utunzaji Mazingira ni jukumu letu sote

*Wafanyakazi Vodacom na Mlimani City waadhimisha siku ya mazingira kwa vitendo
Mhandisi wa Mazingira wa Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira (NEMC), Arnold Kasilaga, akiongea na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wafanyakazi wa Mlimani City. Wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya usafi kwa vitendo kuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,akiongea jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wafanyakazi wa Mlimani City. Wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya usafi kwa vitendokuzunguka maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Mazingira wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira(NEMC), Arnold Kasilaga (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare (katikati), wakimsikiliza jambo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia wakati wa hafla fupi ya  kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mlimani City walifanya kazi ya usafi kwa vitendo kuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka Ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na  wafanyakazi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakifanya usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yanayozunguka ofisi zao  ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani.
Mkuu wa Kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,akiweka uchafu katika moja ya vyombo maalum vya kuhifadhia uchafu baada ya kukusanya uchafu wakati wa kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi kampuni hiyo na pamoja na wafanyakazi wa Mlimani City walifanya kazi ya usafi kwa vitendokuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wafanyakazi wa Mlimani city wakimsikiliza Mhandisi wa Mazingira wa Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira(NEMC)Arnold Kasilaga (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya siku ya mazingira duniani ambapo wafanyakazi hao walifanya kazi ya usafi kwa vitendo kuzunguka maeneo ya Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu
Juni 5, 2015
MHANDISI wa Mazingira kutoka Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira  (NEMC) Bw.Arnold Kasilaga,amesema jukumu la utunzaji mazingira ni la kila mmoja kwa kuwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na binadamu zinachangia kuharibu mazingira.

Bwana Kasilaga aliyasema hayo leo wakati akiongea na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Mlimani City ambao wameshirikiana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka ofisi zao ikiwemo viwanja vya eneo maarufu la biashara na Mikutano ya Kimataifa la Mlimani City.
"Utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila moja hivyo hakikisheni katika shughuli zetu mnazofanya mnatanguliza suala la utunzaji mazingira ama sivyo athari mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa mazingira zitakuwa zikiendelea kujitokeza kila siku"Alisema

Wafanyakazi hao wametumia muda wao kushiriki katika kufagia mazingira,kupanda miti,kusafisha mitaro ya maji machafu na kufyeka nyasi ili kuweka mazingira kwenye hali ya usafi.

Mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare,amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha utunzaji wa mazingira na ndio maana inaipa umuhimu mkubwa siku ya leo ambayo ni siku ya Mazingira Duniani.

Kwetu  Vodacom siku ya leo ni muhimu sana kwa maana tunaamini kuwa utunzaji wa mazingira ni suala muhimu sana katika dunia ya leo na ndio maana tumeamua kuiadhimisha kwa vitendo ambapo wafanyakazi wetu wametumia muda wao kushiriki kazi za usafi,upandaji miti na kutoa elimu ya umuhimu wa kutunza mazingira kwenye vikundi mbalimbali vya jamii”.

Shirika  la Umoja wa Mataifa linaoshughulika na mazingira (UNEP) limetangaza  tarehe 6 ya mwezi Juni  kama Siku ya Mazingira duniani ambapo huadhimishwa kaika nchi mbalimbali duniani kwa kuhimiza utunzaji wa mazingira ambapo makundi mbalimbali hushiriki katika masuala ya kusafisha mazingira na kupanda miti.

Kauli mbiu ya siku ya mazingira Duniani kwa mwaka huu ni Ndoto bilioni saba.Dunia moja.Tumia raslimali kwa uangalifu ambayo inatoa ujumbe kwa kila mmoja anayeishi duniani kuzingatia utunzaji wa mazingira katika kila jambo analofanya.

Kwa hapa nchini maadhimisho haya ya Wiki ya Mazingira ambayo imefikia kilele leo yalizinduliwa rasmi mapema wiki hii na maonyesho ya shughuli za utunzaji mazingira yamefanyika sehemu mbalimbali nchini na  mkoani Tanga ambapo yanaadhimishwa kitaifa.

No comments:

Post a Comment