Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya akieleza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya kuhusu Menejimenti ya Maafa katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam, Juni 4, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Florens Turuka (wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliohudhuria mafunzo ya Menejimenti ya Maafa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Saalaam, Juni 4, 2015.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia) akiteta jambo viongozi wa Ofisi hiyo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenza wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamiliwatu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi na katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya mara baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam Juni 4, 2015.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiiza Mkufunzi wa masuala ya kujikinga na dharura ya moto kutoka Chuo cha Zima moto Bw. Rajabu Mwangalamo wakati wa Mafunzo ya Menejimenti ya Maafa yaliyofanyika Baraza la Maaskofu Kurasini Dar es Salaam Juni 4, 2015.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifanya zoezi la kuzima moto baada ya mafunzo ya kujiandaa na kukabiliana na dharura ya moto Juni 4, 2015 katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofu Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment