TANGAZO


Friday, June 26, 2015

NBAA YATANGAZA MATOKEO

Pius Yalula - MAELEZO
BODI ya Wakurugenzi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kupitia kikao cha 164, imetangaza matokeo ya mitihani iliyofanyika kuanzia Mei 5 hadi 8, 2015, ilifanyika katika vituo 11 vilivyopo Tanzania bara na visiwani.

Taarifa ya matokeo hayo imetolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Bodi NBAA Pius Maneno jana jijini Dar es salaam kwa vyombo vya habari nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matokeo hayo yanahusisha watahiniwa wa hatua ya kwanza na ya pili katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa hesabu (ATEC 1, ATEC 2) zenye masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma; katika ngazi ya utunzaji wa hesabu (ATEC) shahada ya juu ya uhasibu (CPA) ambapo jumla ya watahiniwa 600 wamefaulu mtihani wa shahada ya juu ya uhasibu inchini CPA (T), na kufikia 6,615 tangu mitihani hiyo ianzishwe mwaka 1975.

Katika ngazi ya cheti ATEC 2 inafanya watahiniwa waliofaulu  kufikia 3,565 tangu mitihani ianze mwaka 1991, katika hatua ya awali watahiniwa waliofanya mtihani walikua 365 na waliofaulu  ni 203 ambayo ni  sawa na asilimia 55.6 ya ufaulu na katika hatua ya kati na hatua ya pili watahiniwa waliofanya mtihani ni walikua 3,163 sawa na aslimia 88.0 na kuweza kufaulu katika masomo tofauti tofauti waliyofanya na kwa watahiniwa wa hatua ya mwisho waliofanya mtihani walikua 2,011 sawa na asilimia 93.1 ambao wamefaulu katika baadhi ya masomo waliyofanya.

Aidha, bodi imewapongeza wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka ambao hawakufuzu kutokata tamaa bali waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani ijayo ya bodi.

Kulingana na taratibu za bodi ya NBAA mitihani mingine inatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 3 hadi 6, 2015 na matokeo hayo yanapatikana katika tovuti ya bodi hiyo kupitia wavuti ya www.nbaa-tz.org

No comments:

Post a Comment