TANGAZO


Friday, June 26, 2015

Rais Jakaya Kikwete kufunga mafunzo ya Maofisa Magereza kesho

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Na Pius Yalula - Maelezo, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasimi katika sherehe za kufunga mafunzo ya Maofisa wa Ngazi ya Juu Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ambayo yamechukua muda wa miezi minne yalikuwa na lengo kuwandaa maafisa ambao watashika nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya Jeshi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ,jumla ya wahitimu 104 wamehitimu ambapo kati yao wanaume 76 na wanawake 18 wanatoka Tanzania bara na Wanaume 6,wanawake 4 wanatoka  vyuo vya mafunzo Zanzibar.

Taarifa hiyo imeongeza sherehe hizo zitakwenda sanjari na kuadhimisha siku ya Magereza ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na jeshi la Magereza.

Vilevile sherehe hizo zitahudhuriwa na wakuu wa Magereza toka nchi marafiki ambazo ni Botswana, Kenya, Namibia, Swaziland, Uganda na Zambia.

Katika sherehe hizo mgeni rasmi atakuwa na shughuli ya kukagua gwaride rasmi la wahitimu, atatoa vyeti kwa wahitimu waliofanya vizuri na kuvisha cheo kwa wahitimu.

No comments:

Post a Comment