Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya wateja na walikwa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya NMB Tawi la Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Bwana Abdulla Duchi akitoa neon la shukrani kwa wateja na wananchi walioalikwa na Uongozi wa Benki hiyo katika futari ya pamoja hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas akielezea mikakati ya Benki hiyo mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la Zanzibar hapo Kilimani.
Balozi Seif aliyepo kati kati kwa waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya NMB Makao Makuu Dar es salaa na Tawi la Zanzibar.
Kulia ya
Balozi ni Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikha Fadhil Suleiman Soraga,
Meneja Mkuu wa Idara inayoshughulikia fedha ya NMB Bwana Waziri Banabas,
kushoto ya Balozi ni Meneja wa huduma kwa wateja wa NMB Bwana Majid na Mstahiki
Meya wa Mji wa Zanzibar Khatib Abdulrahman Khatib.
Balozi Seif akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mara baada ya kukamilika kwa futari ya pamoja.
Balozi Seif akiagana na Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB hapo Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mara baada ya kukamilika kwa futari ya pamoja.
Na Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/6/215.
BENKI ya
kuhudumia wateja wadogo wadogo Tanzania (NMB) imeahidi kuendelea kutoa huduma
za Kijamii katika maeneo mbali mbali Nchini Tanzania ili lengo la kuanzishwa
kwake liweze kufikiwa kwa ufanisi.
Meneja Mkuu
wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki Hiyo Bwana Waziri Banabas
alitoa ahadi hiyo wakati Uongozi wa Benki hiyo Tawi la Zanzibar ulipowaandalia
futari ya pamoja baadhi ya wateja wake, Viongozi wa Taasisi tofauti Nchini pamoja
na Wananchi.
Futari hiyo
ya pamoja iliyoandaliwa ndani ya kumi la kwanza la rehema la Mwezi Mtukufu wa
ramadhani imefanyika mara baada ya sala Magharibi
kwa washiriki hao iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini
Zanzibar.
Meneja Mkuu
huyo wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki ya NMB Bwana Waziri
Banabas alisema faida ya fedha zinazokusanywa na Benki hiyo kwa mujibu wa
taratibu iliyojipangia hutolewa katika kusaidia sekta za afya pamoja na elimu.
Bwana
Banabas alifahamisha kwamba kutokana na kukua kwa uchumi wa Zanzibar na
wananchi wake kuhitaji huduma za Kibenki
Uongozi wa NMB una mpango wa kuongeza
Matawi pamoja na ATM ili kukidhi mahitaji ya wananchi hao.
Alisema
Benki ya NMB Hivi sasa ina jumla ya Matawi 17 katika maeneo mbali mbali nchini
Tanzania ambapo mawili kati ya hayo yapo kwa upande wa Zanzibar kiwango ambacho
kinastahiki kuongezwa.
Akigusia
changamoto za uhaba wa vifaa vya maabara katika Maskuli mengi hapa Zanzibar
Meneja Mkuu huyo wa Idara inayoshughulikia masuala ya fedha ya Benki ya NMB
Bwana Waziri Banabas alisema Uongozi wake utazingatia kwa kina tatizo hilo.
Alielezea
matumaini yake kuona kwamba Benki ya NMB italipa kiapaumbele suala hilo kwa nia
ya kulitafutia mbinu na ufumbuzi wa kudumu kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu
wa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Zanzibar.
Bwana Waziri
Banabas amewapongeza Wananchi na wateja wote Nchini Tanzania waliosaidia
kuifanya Benki ya NMB kuwa ya kwanza Tanzania kwa kukusanya shilingi Bilioni
156 mwaka uliopita.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya washiriki wa futari hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Benki ya NMB Kwa kujipangia
utaratibu wa kusaidia huduma za kijamii licha ya jukumu lao la kukusanya mapato.
Balozi Seif
alisema Benki ya NMB imeanzishwa maalum ili kuwapa nguvu Wananchi wa kipato cha
chini kuapata mikopo ya kuwawezesha kiuchumi ili waendeshe maisha yao ya kila
siku kwa matumaini makubwa.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wananchi wote kuitumia Benki hiyo ya NMB katika
shughuli zao za ujasiri amali ambazo ndio njia pekee itakayowakomboa kutokana
na ukali wa maisha.
Alisema NMB yeye binafsi imemuwezesha kujenga mapenzi na
upendo kwa Wananchi wa Jimbo lake la Kitope mara tuu baada ya kuchaguliwa kuwa
Mbunge wao wa Jimbo hilo Mwaka 2005 kwa kupata mkopo mkubwa aliouelekeza katika
kuanzisha miradi ya maendeleo ya Wananchi Jimboni humo.
Uongozi wa
Benki ya NMB tayari umeshafutarisha Wateja na Viongozi wa Kisiwa cha Pemba na
kuahidi kuendeleza utamaduni huo kila mwaka ili kuwapa fursa wateja wake kukaa
pamoja na kubadilishana mawazo na fikra zitakazosaidia kuongeza ufanisi wa
Benki hiyo.
No comments:
Post a Comment