*Kiongozi wa mbio za Mwenge awataka wananchi kujiandikisha Daftari la Wapiga Kura
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe (kushoto) akiwa amekumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Said Magalula baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib (katikati) akipewa maelezo ya zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litakavyoendeshwa, muda mfupi baada ya kuzindua zoezi hilo. (Kulia mwenye tracksuit) ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Betty Mkwasa.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Bw. Juma Khatibu Chum akifungua kitambaa kama ishara ya kuzindua zoezi la uandikishaji wapiga kura Wilayani Mvomero lililofanyika katika Kijiji cha Salawe Kata ya Kibati.
Na Andrew Chimesela (Morogoro)
0719 11 22 99/0785 336 335
(15 Juni, 2015)
Kiongozi wa mbio za Mwenge
wa uhuru Kitaifa Ndugu juma Khatibu Chum amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro
kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kutumia haki yao ya msingi ya
kuchagua viongozi kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Juma Kghatibu ameyasema
hayo leo wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa mkesha wa
mwenge eneo la Kichangani katika Tarafa ya Tuliani Wilayani MvomeroMkoani
Morogoro.
Amesema mwananchi yeyote
ambaye amefikisha umri wa mika 18 na mwenye sifa zote za kuandikishwa aende kujiandikisha ili aweze kupata fursa ya
kuchagua viongozi bora watakaoiongozi nchi katika Serikali ya awamu ya tano.
“Hakuna nchi yeyote
duniani yenye maendeleo bila ya viongozi bora. Na huwezi kupata viongozi bora
nje ya uchaguzi Mkuu. Ni lazima tujiandikisha na kuchagua viongozi bora itakapofika
mwezi Oktoba, uchaguzi ni haki yetu ya kidemokrasia, na ni haki yetu ya
Kikatiba”. alisema Bwana Khatibu.
Mapema akiwa Wilayani
Mvomero ikiwa ni Wilaya ya kwanza kukimbiza mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa
Morogoro, Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa alizindua zoezi la
uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR katika kijiji cha Salawe
kilichoko Kata ya Kibati Wilayani humo tayari kwa zoezi hilo kuanza hapo Juni, 16, 2015.
Aidha, Kiongozi wa Mbio za
Mwenge Kitaifa, alikemea suala la rushwa
akiwataka wananchi kuacha kupokea rushwa kwa kuwa inasababisha kuwapata
viongozi wabovu.
Pia, alisisitiza kutumia vyandarua kadri ya
malengo ya serikali ili kupambana na malaria badala ya kutumia vyandarua hivyo
kwa malengo tofauti.
Kuhusuna ugonjwa hatari wa
Ukimwi, alisema waliokwisha ambukizwa ugonjwa
huo ni vema kuanza kutumia dawa za ARV na kula vyakura bora mapema na kufuata
ushauri unaotolewa na madaktari.
Awali akipokea Mwenge wa
Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Rajabu Rutengwe alibainisha kuwa jumla ya
miradi 51 itapitiwa na mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Morogoro. “Mwenge wa Uhuru ukiwa ndani ya Mkoa wa Morogoro
utakimbizwa ndani ya Wilaya 6 ukipitia jumla ya miradi 51 yenye thamani ya
shilingi 9,750,540,533.40” Alisema.
Aliongeza kuwa “kati ya
hizo, michango ya wananchi ni shilingi,2,522,160,236.00, Halmashauri 574,640,680.00,
Serikali Kuu 4,734,382,176.40.00 na wafadhili 1,919,357,441.00.
Mwenge wa Uhuru, kesho
utaanza mbio zake Wilaya ya Gairo ambapo utapitia jumla ya miradi sita.




No comments:
Post a Comment